Monday, January 21, 2013

SIMBA YATAKATA OMAN YAIBANJUA AHLI-SIDAB,NYOSSO APATA TIMU OMAN

Mabingwa wa soka Tanzania bara, Simba s.c "wekundu wa msimbazi" wamepata ushindi wao wa kwanza nchini Oman baada ya kuiadabisha Ahli Sidab kwa mabao 2-1 katika mchezo wa kirafiki uliochezwa Oman ambako Simba wamepiga kambi kujiandaa na mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Tanzania bara.

Viungo Kigi Makassy na Amri Kihemba walikuwa mashujaa kwa upande wa Simba baada ya kutupia kambani mabao katika kila kipindi cha mchezo huu.
Makassy alitupia kambani bao la kwanza dakika 21 kabla ya kutolewa nje baada ya kuumia na nafasi yake kuchukuliwa na Amri Kiemba ambaye aliingia na kutupia kambani bao la pili na la ushindi katika dakika ya 68.

Wakati huohuo, baada ya kumrudisha kundini beki Juma Nyosso wiki iliyopita, uongozi wa Simba sasa upo mbioni kumuuza beki Juma Nyoso nchini Oman.
Simba kwa sasa ipo kambini Oman na viongozi wake wapo kwenye mazungumzo na wakala Said Ally aliyeonyesha nia ya kumtafutia timu Nyoso.

Nimeshazungumza na Simba na kila kitu kinaenda sawa, tukifikia mwafaka nitaweka wazi ni timu gani atachezea na kiasi ambacho atauzwa, alisema wakala huyo.

Simba wiki iliyopita walimaliza tofauti zao na Nyoso aliyedaiwa kushuka kiwango na kumlazimisha kuchezea timu B, jambo lililopingwa vikali na beki huyo.


Juma Nyosso

MATOKEO KOMBE LA MATAIFA YA AFRIKA 2013

Kombe la Mataifa ya Afrika |MATOKEO


20 January
Mali1 - 0Niger
S Keita (83)
Nelson Mandela Bay Stadium Attendance (20000)
20 January
Ghana2 - 2Congo DR
E Agyemang-Badu (39)
K Asamoah (48)
TM Mputu (52)
D Mbokani (pen 68)
Nelson Mandela Bay Stadium Attendance (7000)
19 January
Angola0 - 0  Morocco
National Stadium Attendance (25000)
19 January
South Africa 0 - 0  Cape Verde Islands
National Stadium Attendance (50000)

TOTTENHAM YAIDAI MAN U "CHENJI" DAKIKA YA 90

Washikilia usukani wa ligi kuu ya England, Manchester United imeambulia pointi moja baada ya kutoka sare ya bao 1-1 na Tottenham.

Mshambuliaji Robin Van Persie aliiwezesha timu yake ya Manchester United kuongoza kipindi cha kwanza baada ya kufunga bao katika dakika ya 25.

Van Persie alipata goli hilo akiunganisha kwa kichwa krosi ya Tom Cleverly baada ya Welbeck kufanya kazi nzuri.

Man United wakiamini kuwa tayari wamepata ushindi katika mechi hiyo,Tottenham waliendelea kudai Chenji kwa kulisakama lango la Man United na  katika dakika ya 90 ya mtanange huo Climp Dempsey aliwanyanyua mashabiki wa Tottenham waliofurika katika dimba la White Hart Lane.Mpambano huo ulishuhudiwa na mashabiki wapatao 35,956

Matokeo hayo bado yanaiacha Manchester United kuendelea kushika usukani wa ligi hiyo ikiwa na pointi 56, huku ikifuatiwa na Manchester City yenye pointi 51.

Tottenham iko katika nafasi ya nne ikiwa na pointi 41, pointi nne nyuma ya Chelsea yenye pointi 45, ikikakalia nafasi ya tatu ya ligi kuu ya England.

Timu zote nne mpaka sasa zimeshacheza mechi 23.

Van Persie akipiga kichwa kilichoelekea moja kwa moja wavuni

Robin Van Persie akishangilia goli

MshikemshikeDempsey akishangilia goli baada ya kubadili matokeo katika dakika ya 90
Tottenham 1-1 Man U

ARSENAL YAZAMA DARAJANI

Chelsea imeweza kupata pointi tatu muhimu katika kinyang'anyiro cha ligi kuu ya Soka England baada ya kuipasua Arsenal magoli 2-1 katika uwanja wa Stanford Bridge.

Juan Mata alitupia bao la kwanza la Chelsea kabla ya Frank Lampard kuhitimisha machungu ya mashabiki wa Arsenal kwa kufunga bao la pili kupitia mkwaju wa penalti.

Hata hivyo Arsenal kupitia kwa mshambuliaji wake Theo Walcott aliweza kufunga bao zuri, akiwazidi maarifa walinzi wa Chelsea pamoja na mlinda mlango mahiri Peter Cech.

Kipindi cha Arsenal ilizidi kuibana Chelsea ambapo ilipata kona tisa dhidi ya tatu za Chelsea. Hata hivyo mechi hiyo ilimalizika kwa Chelsea kuibuka na ushindi huo wa magoli mawili kwa moja.

Huu ni ushindi wa kwanza kwa Chelsea katika uwanja wake mwaka huu 2013 kati ya mechi nne ilizocheza uwanjani hapo Stanford Bridge.

Wachezaji wa Chelsea wakishangilia goli la kwanza

Torres akijaribu kuwatoka mabeki wa Arsenal

Lampard akipiga penati kuandika bao la pili

Walcott akitupia kambani goli la Arsenal

Walcott akishangilia goli na mchezaji mwenzake Jack Wilshere
Chelsea 2-1 Arsenal