Monday, January 21, 2013

TOTTENHAM YAIDAI MAN U "CHENJI" DAKIKA YA 90

Washikilia usukani wa ligi kuu ya England, Manchester United imeambulia pointi moja baada ya kutoka sare ya bao 1-1 na Tottenham.

Mshambuliaji Robin Van Persie aliiwezesha timu yake ya Manchester United kuongoza kipindi cha kwanza baada ya kufunga bao katika dakika ya 25.

Van Persie alipata goli hilo akiunganisha kwa kichwa krosi ya Tom Cleverly baada ya Welbeck kufanya kazi nzuri.

Man United wakiamini kuwa tayari wamepata ushindi katika mechi hiyo,Tottenham waliendelea kudai Chenji kwa kulisakama lango la Man United na  katika dakika ya 90 ya mtanange huo Climp Dempsey aliwanyanyua mashabiki wa Tottenham waliofurika katika dimba la White Hart Lane.Mpambano huo ulishuhudiwa na mashabiki wapatao 35,956

Matokeo hayo bado yanaiacha Manchester United kuendelea kushika usukani wa ligi hiyo ikiwa na pointi 56, huku ikifuatiwa na Manchester City yenye pointi 51.

Tottenham iko katika nafasi ya nne ikiwa na pointi 41, pointi nne nyuma ya Chelsea yenye pointi 45, ikikakalia nafasi ya tatu ya ligi kuu ya England.

Timu zote nne mpaka sasa zimeshacheza mechi 23.

Van Persie akipiga kichwa kilichoelekea moja kwa moja wavuni

Robin Van Persie akishangilia goli

Mshikemshike



Dempsey akishangilia goli baada ya kubadili matokeo katika dakika ya 90
Tottenham 1-1 Man U

No comments:

Post a Comment