Thursday, August 29, 2013

ETO'O ATUA CHELSEA KWA PAUNDI MIL 7

Mtajiri wa London Chelsea hatimae wamekamilisha usajili wa mshambuliaji hatari wa Anj Makhachkhala Mcameroon Samuel Phils Et'oo, Hii ni baada ya Chelsea kushindwa kumnasa mshambuliaji wa Manchester United Wayne Rooney.
Et'oo amesaini mkataba wa mwaka mmoja kwa makubaliano ya kiasi cha paundi milioni 7 kutoka milioni 17 za hapo awali.
Et'oo aliwasili jana usiku jijini London katika stesheni ya Mtakatifu Pancras (St Pancras) . Et'oo mwenye umri wa miaka 32 sasa atafanyiwa vipimo vya afya katika viwanja vya mafunzo vya Chelsea vya Cobham kabla ya kumalizia taratibu zingine za usajili leo hii baadae.
 Samuel Eto'o
Samuel Et'oo
Eto'o akiwa London tayari kukamilisha usajili wake na Chelsea.

4
5
Eto'o akiwa ndani ya Taxi dakika chache baada ya kuingia London usiku wa jana.
Et'oo muda mchache baada a kuwasili London

BREAKING NEWZZ!! MAJAMBAZI YAVAMIA BENKI KARIAKOO NA KUPORA FEDHA KIBAO

Watu wanaodhaniwa kuwa ni Majambazi wamevalia sare za Jeshi la Polisi wamevamia Habib Afriican Bank Kariakoo DSM na kupora kiasi kikubwa cha Fedha. Jeshi la polisi kanda maalum wamethibitisha kutokea kwa tukio hilo. Habari kamili itakujia hivi punde......