Monday, November 7, 2011

MIAKA 50 YA UHURU: Hotuba ya hayati Baba wa Taifa Mwl JK Nyerere kwa waandishi wa habari 1995 Dar es salaam

WIMBO WA LEO, DJ Cleo - FACEBOOK

Huyu ndio Moise Katumbi CHAPWE, Rais wa TOUT PUISSANT MAZEMBE


Rais wa TP Mazembe, Moise Katumbi Chapwe akiwa ndani ya ndege inayomilikiwa na klabu hiyo.


Wadau wa TP Mazembe wakipata huduma ndani ya pipa linalomilikiwa na Tout Puisssant Mazembe


Presidaa wa TP Mazembe Moise Katumbi akishuka kutoka kwenye ndege inayomilikiwa na TP Mazembe


Mmoja kati ya wahudumu wa ndani ya ndege ya TP Mazembe


Rais wa TP Mazembe Moise Katumbi Chapwe akichekelea ndani ya ndege


Baadhi ya wadau wa TP Mazembe


Wachezaji na wadau wengine wamejiachia ndani ya dege la TP Mazembe

Ulimwengu apewa tano TP Mazembe( buteur ambitieux )

Thomas ULIMWENGU, buteur ambitieux
Thomas Ulimwengu

KLABU ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia, imesema inamkubali mshambuliaji wa timu hiyo, Thomas Ulimwengu kuwa ni mchezaji mwenye uchu wa kufunga kila mara anapolitazama lango.

Kwa mujibu wa mtandao wa klabu hiyo, 'dogo' huyo wa Tanzania, aliingizwa kwenye mchezo wa timu hiyo na Don Bosco katika dakika ya 81 dhidi ya Don Bosco, na ilimchukua dakika tatu kufunga bao.

Mshambuliaji huyo anayefikisha miaka 18 Juni 14 mwakani na mzaliwa wa Dodoma, aliitwa kwenye timu ya U-17 baada ya kupata mafunzo katika shule ya TSA.

Tovuti hiyo ilimwelezea Ulimwengu kuwa ukali wake unatokana na kuwemo katika mashindano ya U-17 na hata kuibuka mfunaji bora wa michuano ya Cecafa 2009.

Ulimwengu alikuwa mmoja wa wachezaji walioibuliwa na Marcio Maximo, na mara kadhaa amekuwa akimtumia katika safari mbalimbali za Taifa Stars ili kupata uzoefu.


Thomas Ulimwengu kazini TP Mazembe

Bolton yafanya maangamizi,Tottenham yailowesha Fulham

Bolton yazinduka kutoka usingizini

Chris Eagles na Ivan Klasnic walipachika mabao mawili kila mmoja wakati Bolton ilipoisasambua Stoke City na kuweza kupata ushindi wao wa kwanza nyumbani msimu huu na kujiondoa katika mizizi ya msimamo wa ligi
Kevin Davies alifunga bao la kwanza lililoonekana ni la utata ndani ya sekunde 90 baada ya kupigwa free-kick ya haraka na Klasnic.

Bolton vs Stoke City
Eagles alipachika bao la pili kwa mkwaju maridadi baada ya Asmir Begovic kushindwa kuweka mpira wavuni.

Klasnic alifumua mkwaju mkali umbali wa yadi 18 na kuandika bao la tatu kabla ya Eagles kufunga bao la nne na Klasnic akapachika bao la tano kwa kichwa na kukamilisha kazi ya ushindi maridadi.

Matokeo hayo yalikuwa ni nafuu kwa Bolton ambayo imeanza msimu huu kwa kusuasua.

Wolves nayo ilimaliza ukame wa kukosa ushindi kwa mara ya nane mfululizo baada ya kuilaza Wigan mabao 3-1.

Walikuwa Wolves walioanza kuliona lango la wageni wao Wigan katika dakika ya 31 kwa bao la Jamie O'Hara baada ya kuunganisha pasi kutoka kwa Kevin Doyle.

Lakini Ben Watson aliisawazishia Wigan, baada ya kuunganisha mpira uliookolewa na mlinda mlango Wayne Hennessey ambaye awali aliokoa mkwaju wa penalti.

David Edwards aliihakikishia mwendo mzuri Wolves kwa kuandika bao la pili kwa mkwaju wa karibu na Stephen Ward akahitimisha mabao kwa kufunga bao la tatu.

Ushindi huo ni mzuri kwa Wolves ambao wananuia kujinasua kutoka eneo la kushuka daraja.

Lakini Wigan inaendelea kubakia mkiani mwa msimamo wa ligi na wamo katika matatizo makubwa baada ya kuweka rekodi mpya ya klabu hiyo ya kushindwa michezo minane mfululizo katika Ligi Kuu ya England. Hakuna timu ambayo ilikuwa na rekodi kama hiyo na ikaweza kuepuka kushuka daraja.


Tottenham imeweza kucheza mechi yao ya kwanza ya ligi bila ya meneja wao Harry Redknapp na kufanikiwa kupata ushindi murua katika uwanja wa Fulham kwa kuilaza mabao 3-1 ukiwa ni ushindi wao wa nane mfululizo wa ligi msimu huu.

Redknapp hakuwepo uwanjani wakati huu akiwa anaendelea kujiuguza nyumbani kwake baada ya kufanyiwa upasuaji mdogo wa moyo mapema wiki hii.

Gareth Bale alikuwa wa kwanza kuifungia Tottenham bao la kwanza baada ya kufumua mkwaju mkali uliomchanganya mlinzi wa Fulham Chris Baird kabla ya Aaron Lennon kufunga bao maridadi la pili baada ya kuipangua ngome ya Fulham.

Fulham walipata bao lao moja baada ya mlinzi wa Tottenham Younus Kaboul kujifunga mwenyewe, kabla Jermain Defoe kuithibitishia ushindi timu hiyo kwa kuandika bao la tatu.

Mn City yapaa,Arsenal yaua,Man United na Chelsea zashinda kwa mbinde

Man City ilipoilaza QPR

Man ilipoifunga Sunderland

Chelsea ikiivurumisha Blackburn bakora 1 kwa uchungu

Arsenal ikiilaza WBA 3-0
KLABU ya Manchester City imeendelea kujisafishia njia kuelekea kwenye ubingwa wa Ligi Kuu ya England baada ya juzi kuilaza Queens Park Rangers mabao 3-2.

Alikuwa Yaya Toure aliyeanza kufumania nyavu katika dakika ya 16 ikiwa ni sehemu ya ushindi huo ulioiacha Manchester United kwa pointi tano zaidi.

Manchester United iliyokuwa imeikaribia timu hiyo kwa pointi, lakini mabao ya Edin Dzeko na David Silva yalifutwa na Jay Bothroyd na Heidar Helguson, na lile la Toure alilofunga kwa kichwa akiunganisha mpira wa Alexsandr Kolarov na kuifanya timu hiyo kushinda mechi yake ya 10 mfululizo.

United ilimzawadia kocha wao Sir Alex Ferguson ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Sunderland. Ferguson alitimiza miaka 25 jana akiwa kocha wa timu hiyo.

Nayo Chelsea iliibuka na ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Blackburn.

“Ilikuwa siku nzuri kwetu,” alisema Ferguson. “Nilikuwa nina wasiwasi timu isingeweza kufanya vizuri. Nilidhani bado timu ina 'mawenge' ya kufungwa. Wakati mwingine lazima uwe na wasiwasi huu, hali iliyokuwa nayo, lakini tumeshinda.”

Ushindi wa timu hiyo uliwezeshwa na beki wa timu hiyo, Wes Brown aliyejifunga akiwa katika harakati za kuokoa. Beki huyo aliyekuwa Man. United, alijiunga na timu hiyo mapema Julai.

Ferguson alikwenda katikati ya uwanja ni kama alikuwa akikagua gwaride la wachezaji wa United na Sunderland. Mashabiki 75,570 walimpigia makofi Ferguson huku bosi wa klabu hiyo, David Gill akitangaza kuwa jukwaa la upande wa kaskazini mwa uwanja litaitwa jina la kocha huyo.

“Sikutarajia hili,” Ferguson alisema. “Ni kama wamenishtukiza.”

Chelsea ilipata bao lake kupitia kwa Frank Lampard katika dakika ya 50 huku ikiisogelea United. Newcastle imeendeleza wimbi la ushindi kwa kuichapa 2-1 Everton. Arsenal nayo iliizamisha West Bromwich Albion mabao 3-0.