Monday, November 7, 2011

Ulimwengu apewa tano TP Mazembe( buteur ambitieux )

Thomas ULIMWENGU, buteur ambitieux
Thomas Ulimwengu

KLABU ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia, imesema inamkubali mshambuliaji wa timu hiyo, Thomas Ulimwengu kuwa ni mchezaji mwenye uchu wa kufunga kila mara anapolitazama lango.

Kwa mujibu wa mtandao wa klabu hiyo, 'dogo' huyo wa Tanzania, aliingizwa kwenye mchezo wa timu hiyo na Don Bosco katika dakika ya 81 dhidi ya Don Bosco, na ilimchukua dakika tatu kufunga bao.

Mshambuliaji huyo anayefikisha miaka 18 Juni 14 mwakani na mzaliwa wa Dodoma, aliitwa kwenye timu ya U-17 baada ya kupata mafunzo katika shule ya TSA.

Tovuti hiyo ilimwelezea Ulimwengu kuwa ukali wake unatokana na kuwemo katika mashindano ya U-17 na hata kuibuka mfunaji bora wa michuano ya Cecafa 2009.

Ulimwengu alikuwa mmoja wa wachezaji walioibuliwa na Marcio Maximo, na mara kadhaa amekuwa akimtumia katika safari mbalimbali za Taifa Stars ili kupata uzoefu.


Thomas Ulimwengu kazini TP Mazembe

No comments:

Post a Comment