Thursday, December 5, 2013

MSIMAMO WA LIGI KUU YA UINGEREZA BAADA YA MECHI ZA JANA USIKU
 
Position Team Played Goal Difference Points
1 Arsenal 14 19 34
2 Chelsea 14 14 30
3 Man City 14 26 28
4 Liverpool 14 13 27
5 Everton 14 9 27
6 Tottenham 14 -2 24
7 Newcastle 14 -2 23
8 Southampton 14 5 22
9 Man Utd 14 4 22
10 Aston Villa 14 0 19
11 Swansea 14 1 18
12 Hull 14 -6 17
13 West Brom 14 -2 15
14 Stoke 14 -6 14
15 Cardiff 14 -9 14
16 Norwich 14 -16 14
17 West Ham 14 -3 13
18 Fulham 14 -14 10
19 Crystal Palace 14 -14 10
20 Sunderland 14 -17 8

ARSENAL MOTO CHINI, LIVERPOOL,MAN CITY KICHEKO, MAN UTD CHALIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIII

Arsenal imeendeleza wimbi la ushindi na kukomaa kileleni mwa ligi kuu ya Uingereza kwa kuichabanga Hull City kwa bakora 2 kwa uchungu katika dimba la Emirates jana usiku.
Dakika ya pili ya mchezo Mchezaji wa Denmark Nichlas Bendtner alitoa gundu la kutokufunga magoli kwa kichwa safi akiunganisha krosi iliyopigwa na Jenkinson.


Nicklas Bendtner akishangilia baada ya kufunga goli la kwanza

Mpaka timu zinaenda mapumziko Arsenal ilikuwa ikiongoza kwa bao 1-0. Kipindi cha pili kiliendelea kuwaumiza Hull City wakati vijana wa Wenger wenye morali ya hali ya juu mwaka huu na matumaini ya kunyakua ndoo ya ligi kuu ya Uingereza, ilikuwa dakika ya 47 ya mchezo pale mchezaji ghali kuliko wote Arsena Metsut Ozil alipotupia mpira kambani baada ya kazi nzuri iliyofanywa na Aaron Ramsey.
 
Ozil akitupia kambani goli la pili dk 47

 
Ozil kazini 
ARSENAL 2-0 HULL CITY

Katika mchezo mwingine wa ligi kuu Uingereza ilishuhudiwa Liverpool wakifanya mauaji kwa kuiadhibu Norwich City kwa bakora 5-1 katika dimba la Anfield. Luis Suarez hakuridhika na Hat-Trick na badala yake akatupia kambani mabao manne huku moja likitupiwa kambani na kijana mdogo Raheem Sterling na lile la kufutia machozi la Norwich lilitupiwa kambani na Bradley Johnson.


Luis Suarez akishangilia goli.


Suarez akitupia kambani goli la nne


Suarez na Gerrald katika furaha ya ushindi.
 
LIVERPOOL 5-1 NORWICH CITYKatika mchezo mwingine ilishuhudiwa Man United wakiangukia pua kwa kuchabangwa bao 1-0 na Everton, goli pekee la mchezo huo likitupiwa kambani na Brian Oviedo dk 85.

Brian akitupia kambani bao pekee huku kipa wa Man Utd David De Gea akiwa hana ujanja.


Wachezaji wa Everton wakishangilia ushindi dhidi ya Man Utd hapo jana usiku.

 
MAN UTD 0-1 EVERTON


MATOKEO YA MECHI ZA JANA
Jumatano 4 Des 2013 - LIGI KUU UINGEREZA