Monday, September 5, 2011

MAMBO YA UFUKWENI NI NOUMAAA

  •  

750,000 KUFA NJAA SOMALIA

Watu zaidi ya 750,000 huenda wakafa njaa kutokana na makali ya ukame katika miezi inayokuja, hii ni onyo iliyotolewa na Umoja wa Mataifa ikitangaza njaa katika eneo jingine jipya.
Umoja wa Mataifa unasema maelfu ya watu wamekufa baada ya kile kinachotajwa kuwa ukame mbaya zaidi kuikumba Afrika Mashariki katika kipindi cha miaka 60.
Eneo la Bay limetajwa kama eneo la sita kutangazwa rasmi kuwa na njaa katika sehemu za kusini mwa Somalia zinazotawaliwa na wapiganaji wa al Shabab.
Umoja wa Mataifa unasema watu milioni 12 katika eneo hilo wanahitaji msaada wa chakula.
Kwa jumla watu milioni 4 wanakabiliwa na matatizo ya chakula Somalia ambapo watu 750,000 wako katika hatari ya kufa katika miezi minne ijayo kutokana na ukosefu wa msaada unaohitajika kwa dharura
Njaa Somalia 
Tamko la idara ya chakula na ufafanuzi wa lishe bora-FSNAU.
Idadi ya watu wanaokufa katika eneo la Bay sasa imefika idadi ambayo inaliorodhesha eneo hilo kutangazwa rasmi kuwa linakabiliwa na njaa.
Nchi jirani za Djibouti, Eritrea, Ethiopia, Kenya na Uganda pia zinatatizika kutokana na ukosefu wa mvua.
Mwandishi wa BBC katika eneo la Afrika Mashariki Will Ross anasema kuwa ni vigumu sana kwa mashirika ya misaada ya kibinadamu kuwafikia watu katika maeneo yanayokaliwa na wapiganaji wa al Shabab.
Kundi hilo la al Shabab linalohusishwa na Al Qaeda linadhibiti eneo kubwa la kusini mwa Somalia ikiwa ndio sehemu iliyokabiliwa vibaya na ukame nchini humo.
Baadhi ya maafisa wa al Shabab wameyashutumu mashirka ya misaada kutoka mataifa ya magharibi kuwa yanaongeza chumvi kuhusu hali halisi ya mambo kwa malengo yao ya kisiasa.
Mwandishi wa BBC anasema kiasi cha msaada wa chakula kinafika katika sehemu hiyo lakini sio kwa kiwango kinachohitajika.

BOLT NI NOMA

Usain Bolt ameiongoza Jamaica kuweka rekodi mpya ya dunia ya sekunde 37.04 wakati waliposhinda mbio za mita 4x100 kwa wanaume kupokezana vijiti wakati wa siku ya mwisho ya mashindano ya riadha ya Dunia mjini Daegu.
Timu hiyo Ya Jamaica, iliyojumuisha pia bingwa mpya wa dunia wa mbio za mita 100 Yohan Blake, iliishinda timu ya Ufaransa na St Kitts and Nevis.
Timu ya Marekani ilishindwa kumaliza baada ya mkimbiaji wake mmoja kuanguka baada ya kugongana na mkimbiaji wa Uingereza, ambaye alikiangusha kijiti wakati wa kumkabidhi mwenzake.
Maria Savinova
Maria Savinova
Naye Mariya Savinova wa Urusi naye alimaliza vizuri na kumshinda Caster Semenya wa Afrika Kusini katika fainali ya mbio za mita 800 wanawake.