Tuesday, April 29, 2014

ARSENAL YAISAMBARATISHA NEWCASTLE 3-0

Arsenal ya Uingereza ilijiweka katika nafasi nzuri ya kufuzu kwa mchuano wa ligi ya mabingwa mwakani baada ya kuinyuka Newcastle mabao matatu kwa nunge katika mechi ya katikati ya juma iliyochezwa katika uwanja wao wa nyumbani wa Emirate.
 
Koscielny akitupia kambani bao la kwanza
 
 
Giroud akimpongeza Koscielny baada ya kufunga goli la kwanza

Ushindi huo umeiacha Arsenal na jumla ya alama 73 nne zaidi ya wapinzani wao wa karibu Everton wenye alama 69.
Laurent Koscielny ndiye aliweka niya ya 'the Gunners' bayana alipofunga mkwaju wa Santi Cazorla kunako dakika ya 26 ya kipindi cha kwanza . Mesut Ozil naye akaongezea la pili kabla ya kukamilika kipindi cha kwanza .
Hata hivyo ni Olivier Giroud ndiye aliyemhakikishia kocha Arsene Wenger alama tatu muhimu alipohitisha kichapo hicho kwa bao la tatu kunako dakika ya 66 ya mechi hiyo.
Aidha ilikuwa ni kichapo cha 6 mfululizo kwa timu ya Newcastle na kocha Alan Pardew .
Hata hivyo mbivu na mbichi itabainika Manchester City itakapokwaruzana na Everton jumamosi ijayo.
Timu nne za kwanza ndizo zinazoshiriki mchuano huo wenye kitita kikubwa zaidi barani.
Arsenal ilikuwa imedorora kutoka nafasi ya kwanza na ilikuwa na hatari ya kukosa kushiriki ligi hiyo.
 
Ozil akishangilia kutupia bao la pili


Mshikemshike kwenye lango la Newcastle


Refa nipe penatiiiiiiii
 
ARSENAL 3-0 NEWCASTLE