Galatasaray imemsajili aliyekuwa mshambulizi wa Chelsea Didier Drogba kutoka
kwa klabu ya Shanghai Shenhua inayoshiriki katika ligi kuu ya Premier nchini
Uchina.
Galatasaray inayocheza ligi kuu nchini Uturuki, imethibitisha kuwa Drogba
amesaini mkataba wa miezoi kumi na minane na klabu hiyo.
Mchezaji hiyo mwenye umri wa miaka 34, kwa sasa yuko nchini Afrika Kusini
kuiongoza kikosi cha Ivory Coast katika mashindano ya kuwania kombe la mataifa
ya Afrika.
Kwa mujibu wa ujumbe uliotumwa na kampuni ya uhusiano bora inayomuakilisha
mchezaji huyo Sports PR Company na kuchapishwa kwa mtandano wa kijamii wa
Twitter, Drogba alisema anajiandaa kurejea tena katika michuano ya kuwania kombe
la klabu binga barani ulaya kwa mara nyingine.
Galatasaray imefuzu kwa raundi ya muondoana ya kuwania kombe hilo na
imepangiwa kucheza na FC Schalke 04 kutoka uUjerumani.
''Hii ni fursa nzuri ya kuichezea timu kubwa na ni nafasi ambayo siwezi
kupuuza'' Alisema Drogba.
Agenti wam mchezaji huyo amesema, Drogba atajiunga la klabu hiyo ya
Galatasaray baada ya kukamilika kwa michuano ya kuwania kombe la mataifa ya
Afrika.
Drogba ni mchezaji wa pili wa hadhi ya juu kusajiliwa na Galatasaray baada ya
Wesley Sneijder aliyejiunga na klabu hiyo kutoka klabu ya Inter Milan.
Drogba alijiunga na Shanghai Shenhua mwezi juna mwaka uliopita na ameifunga
jumla ya magoli manane baada ya kucheza mechi kumi na moja.
Awali Drogba alitaka kurejea Ulaya kwa mkopo na klabu yake ya zamani ilikuwa
imeanzisha mazungumzo ya kumsajili.
Lakini shirikisho la mchezo wa soka duniani FIFA lilipinga uhamisho huo,
likisema kuwa linakiuka sheria za kimataifa kuhusu uhamisho na usajili wa
wachezaji.
Mchezaji mwingine wa zamani wa Cheslea Nicolas Anelka huenda pia anajiandaa
kukihama klabu hiyo ya Shenhua, baada ya kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu
katika klabu ya Juventus.
Drogba katika uzi wa Shenhua
Wesley Sneijder
BALOTELLI ATUA AC MILAN
Mkurugenzi wa klabu ya AC Millan, Umberto Gandini amethibitisha kuwa klabu
hiyo imemsajili mshambuliaji wa Manchester City Mario Balotelli kwa mkataba wa
miaka minne na nusu.
Balotelli, 22, anatarajiwa kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu mjini Milan siku
ya Jumatano kabla ya kusaini wake na klabu hiyo.
Inakisiwa kuwa AC Milan imemsajili mchezaji huyo kwa kitita cha pauni milioni
20.
Awali Manchester City ilianzisha mazungumzo na vilabu vya AC Milan na
Juventus kuhusu uwezekano wa kumsajili mshambuliaji wake Mario Balotelli, na
ripoti zinasema kuwa, Balotelli atauzwa ikiwa vilabu hivyo vitaweza kulipa fedha
wanazo taka.
Klabu hiyo imesema mchezji huyo mwenye umri wa miaka 22, anakisiwa kugharibu
pauni milioni ishirini na moja mbali na fedha zingine za ziada.
Balotelli hana haraka ya kuuzwa na Manchester City imesema haina mipango ya
kupunguza mshahara wake ili aondoke.
Kinyume na matarajio ya wengi Balotelli amesafiri na wachezaji wa Manchester
City watakaocheza na QPR katika mechi ya ligi kuu ya premir leo usiku.
Milan ilianzisha mazungumzo na Man City, kuhusu mchezaji huyo kutoka Italia
na kuna ripoti kuwa klabu ya Juventus vile vile imewasilisha ombi la kutka
kumsajili Balotelli, ambaye alijiunga na Manchester City Agosti mwaka wa 2010
kwa kitita cha pauni milioni 24.
Mario Baruah Balotelli
Swaga za kitaani
Mapema siku ya Jumatatu, naibu kocha mkuu wa Man City, David Platt, alisema
kuwa Balotelli hatajiunga na AC Millan mwezi huu.
Siku ya Ijumaa wiki iliyopita, kocha wa Man City Roberto Mancini, alikariri
hana nia ya kumuuza kuwa mchezaji huyo kutoka Italia.
Balotelli ambaye amefunga goli moja baada ya kucheza mechi kumi na nne msimu
huu, amekumba na kashfa nyingi tangu aliposajiliwa.
Tukio la hivi karibuni, likiwa mzozo kati yake na Mancini katika uwanja wao
wa mazoezi mwanzo wa mwezi huu.
Makamu wa rais wa AC Milan Adriano Galliani amesema ikiwa Manchester City
itapunguza bei ya mchezaji huyo, basi huenda wakamsajili.