Wednesday, January 30, 2013

SHABIKI AKOJOLEA NDINGA YA BALOTELLI


Shabiki anayesadikiwa kuwa Man United akikojolea ndinga ya Balotelli


Baada ya kuikojolea mwingine akashusha suruali na akapanda nyuma ya "Boneti"

Gari aina ya Bentley yenye thamani ya paundi za Uingereza 160,000 inayomilikiwa na mshambuliaji mtukutu wa Manchester City ambae kwasasa amesajiliwa na AC Milan Mario Bawuah Balotelli, ilikojolewa na mtu anayeasadikiwa kuwa ni shabiki wa Manchester United ilipokuwa imepaki katika mgahawa ujulikanao kama Indian Restaurant Zouk uliopo katikati ya jiji la Manchester siku ya Jumapili jioni.

Shabiki mwingine alionekana akiungana na mwenzake kulifanyia uhalifu gari la Balotelli kwa kushusha suruali yake na kupanda nyuma ya Boneti huku akipiga kelele.
Shuhuda wa tukio hilo Michael Armorgie aliliambia gazeti la The Sun kuwa "Nilikuwa ninapita ndipo nikawaona vijana wawili wakifanya vituko kwenye gari la Balotelli,Sikuamini..mmoja alikuwa analikojolea na mwingine amepanda juu anaimba nyimbo za Manchester United".

Hii ndio ndiga ya Balotelli iliyokojolewa

No comments:

Post a Comment