Thursday, September 20, 2012

CHELSEA YAGAWANA POINTI NA JUVENTUS, MAN U YAIBURUZA GALATASARAY

Oscar akishangilia goli pamoja na wenzake Ramires na David Luiz
 
Mabingwa watetezi wa klabu bingwa barani Ulaya, Chelsea ya Uingereza, wakiwa katika dimba la nyumbani la Stamford Bridge, walishindwa kuifunga Juventus ya Italia katika pambano la Jumatano usiku.

Nyota wa Chelsea alikuwa ni mchezaji Oscar kutoka Brazil, ambaye alifanikiwa kutumbukiza magoli mawili kambani katika kipindi cha kwanza; dakika ya 31 na 33.
Bao la pili liliingia kupitia mkwaju wa mbali, na ambalo lilimuacha kipa wa Juventus, Gianluigi Buffon akiwa amezubaa.
Oscar alisajiliwa na Chelsea hivi majuzi.


Hata hivyo Juventus, mabingwa wa Italia, na ambao hawakushindwa katika mechi 42 za Serie A huko nyumbani, walijikakamua na hatimaye kusawazisha na kujinyakulia pointi moja.

Arturo Vidal aliwafungia bao kabla ya kipindi cha kwanza kumalizika, na baadaye mchezaji wa zamu, Fabio Quagliarella, zikiwa zimesalia dakika tisa mechi kumalizika, alithibitisha Juventus ilikuwa na nia ya kuondoka na angalau pointi moja.


Oscar akifunga goli katika mechi dhidi ya Juventus


Oscar akimdhibiti mkongwe Andre Pirlo


Oscar akitupia Kamba ya pili


Wachezaji wa Juventus wakishangilia goli la kusawazisha


Torres akiwa chini ya ulinzi mkali


Kazi kweli kweli ..Lampard amekamwata

Kati ya mechi nane za Jumatano, Manchester United pia ilikuwa uwanjani kupambana na Galatasaray, na vijana wa Sir Alex Ferguson wakichezea nyumbani, mechi ya kundi G, walipata ushindi wa bao 1-0.
Michael Carrick aliandikisha bao hilo mapema, dakika ya 7.

Klabu hiyo ya Uturuki itadhaniwa na wengi kwamba ilinyimwa nafasi ya kusawazisha, kwa mwamuzi kuwapa penalti, baada ya Nemanja Vidic kumchezea vibaya Umut Bulup.



Picha zikionesha jinsi Carrick alivyomtesa mlinda mlango wa Galatasaray na kutia mpira kambani.

Wachezaji wa Man U wakimpongeza Carrick