Wednesday, November 16, 2011

Diamond-Buy it all

Picha za mwanga wa Radi zilizowahi kushangaza zaidi duniani

1
Mpiga picha Mike Tan alipiga picha hii karibu na Polson Pier. katika mahojioano Mike alisema"Kwa muda huo ilikuwa inatisha zaidi kuona radi inapiga karibu na sio zaidi ya kilomita tano,lakini nikasahau hatari ili mradi nipate picha"

1

Thunderstorm Rolls Through Las Vegas

A lightning bolt strikes near the Dubuque County Fair Wednesday night, July 27, 2011 during a storm in Dubuque, Iowa. Dubuque County was under a tornado warning Wednesday night. (AP Photo/The Telegrap

Lightning strikes over the Puyehue volcano, over 500 miles south of Santiago, Chile, Monday June 6, 2011.  Authorities have evacuated about 3,500 people in the nearby area. The volcano was calm on Mon

1

1

NASA has set October 28 for its planned launch of a satellite to help weather forecasters predict extreme storms

1

1

1

Lightning spreads across the sky over the Russian Orthodox Church of Three Saints in Garfield, N.J., during a storm on Thursday, Aug. 18, 2011. (AP Photo/Julio Cortez)

1

1

1

1

Lightning strikes over a church tower during a thunderstorm in Zurich

Lightning strikes over Palmdale, Calif., early Tuesday Oct. 19, 2010 as a low pressure system brings unsettled wet weather to Southern California. (AP Photo/Mike Meadows)

Lightning strikes behind the Mandalay Bay and Luxor hotel casinos as a thunderstorm passes through Las Vegas
Hizi ndio picha za mwanga wa radi za kushangaza zaidi kwa mwaka wa 2011

African Stars Band(Twanga Pepeta)-Aminata

THIS IS DAR ES SALAAM CITY,TANZANIA (Hili ni jiji la Dar es salaam,TANZANIA)


These are Dar es salaam City center photos opposite Kigamboni peninsula,Dar es salaam is among the top 10 rapid growing cities.
Photos by Stuart on Flickr.

TANZANIA TOURIST ATTRACTIONSThe Road across Rift Valley in Tanzania


One of the peak of Mt Kilimanjaro,Mt Meru


Clouds beauty at Mt Kilimanjaro


Mount Kilimanjaro


The highest mountain in Africa,Mount KilimanjaroHippo in the Grumet RiverA Lion at Kirawira

Mtambo wa TANESCO wa kusambaza umeme Dar waunguaKikosi cha zima moto

MOTO mkubwa umezuka jana kwenye Makao Makuu ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) na kuunguza kifaa kiitwacho ‘reactor’ kinachotumika kudhibiti mfumo wa usambazaji umeme katika jiji la Dar es Salaam hali iliyosababisha jiji hilo kukosa umeme.Tukio hilo lililotokea saa 10:45 jioni, lilisababisha kukatika kwa umeme katika jiji hilo na viunga vyake huku uongozi wa ukisema haijajulikana tatizo hilo lingechukua muda gani kutatuliwa.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco, Sophia Mgonja aliwaambia waandishi wa habari kwamba: “Hadi sasa hatujui chanzo na wala athari zake. Umememe umekatika jiji zima na hatuwezi kurudisha hadi tutakapofanya uchunguzi kuona kiwango cha uharibifu.”

Alisema kifaa hicho kilichoungua kinachokadiriwa kuwa na thamani ya Dola za Marekani 500,000 (takriban Sh 900milioni) hakitengenezeki na badala yake kinatakiwa kuagizwa kingine.

Mgonja alisema mbali ya kifaa hicho vingine kama ‘Control Cable’ pamoja na vikombe vya kwenye nguzo ambavyo vilikuwa havionekani kutokana na kufunikwa kwa moshi huenda navyo vimeteketea.“Kuanzia sasa mafundi wanaanza kazi ya kuchunguza chanzo cha tukio hilo lakini pia kuona namna tunavyoweza kurudisha umeme kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam”.

Mkuu wa zamu wa Kikosi wa Kikosi cha Zimamoto wa Jiji la Dar es Salaam, Seleman Said alisema kikosi hicho kiliwasili katika eneo hilo saa 11:03 baada ya kupata taarifa saa 10:45 jioni.

Alisema baada ya kuwasili, walielezwa kuwa kifaa hicho kina mafuta hivyo kulazimika kuchanganya maji na dawa ili kuwezesha kazi hiyo kufanywa kwa ufanisi.“Kazi tuliifanya kwa muda wa dakika saba na katika muda wa dakika 20 tulikuwa tunamalizia kuhakikisha moto huo haulipuki tena,” alisema Said

Taifa Stars yachapwa yasonga mbele kukutana na Ivory Coast,Kenya yafanya mauaji

Stars
Timu ya Taifa ya Kenya,Harambee Stars

Kenya imefuzu kuingia katika ngazi ya makundi ya kufuzu kucheza Kombe la Dunia 2014 kwa kuizaba Ushelisheli 4-0 siku ya Jumanne.
Harambee Stars inasonga mbele kwa kupata mabao 7-0 ya jumla baada ya kupata ushindi wa 3-0 katika mchezo wa kwanza kwenye uwanja wa Nyayo jijini Nairobi.
Magoli ya Harambee Stars yamefungwa na Brian Mandela, Dennis Oliech, Titus Mulama na Victor Wanyama. Kenya sasa itapambana na Nigeria, Malawi na Namibia au Djibouti katika kundi F la kufuzu.
Tanzania nayo ilisonga mbele licha ya kufungwa wakiwa nyumbani 1-0 na Chad kwenye uwanja wa Taifa, Dar es Salaam siku ya Jumanne.

Taifa Stars walitarajiwa kupata ushindi mzito kutokana na kushinda 2-1 katika mchezo wa kwanza mjini N'Djamena siku ya Ijumaa.

Lakini Chad waliwashangaza Stars dakika tatu baada ya mapumziko wakati Muhamat Ahmat Labo alipowanyamazisha mashabiki wa Tanzania.

Hata hivyo Tanzania imeweza kusonga mbele kutokana na kanuni ya mabao ya ugenini kwa kuwa timu hizo zilikuwa na matokeo ya jumla ya 2-2.

Taifa Stars sasa ina kibarua kigumu sawa na kugonga kokoto cha kupanda katika ngazi ya makundi kwani inakabiliwa na Ivory Coast, Morocco na Gambia.

Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC) iliendelea kutoa kisago kwa kuigaragaza Swaziland 5-1 mjini Kinshasa siku ya Jumanne na kujihakikishia nafasi katika ngazi ya makundi.

Mabao mawili kutoka kwa Mputu Mabi na mawili kutoka kwa Alain Kaluyituka na moja kutoka kwa Ilunga Diba yalizamisha jahazi la Swaziland. Wanasonga mbele kwa jumla ya magoli 8-2, baada ya kushinda 3-1 katika mchezo wa awali.

DRC itapambana na Cameroon, Libya na Togo katika kundi I la kufuzu.

Togo ilithibitisha nafasi yake katika kundi lao siku ya Jumanne baada ya kuifunga Guinea Bissau 1-0 mjini Lome.

Togo wanasonga mbele kwa jumla ya mabao 2-1. Emmanuel Adebayor alicheza mechi yake ya kwanza katika kipindi cha miaka miwili baada ya kubadili uamuzi wake wa kutoichezea timu yake ya taifa.

Lesotho nayo ilifika katika ngazi ya makundi ya kufuzu kucheza Kombe la Dunia 2014 licha ya kupoteza mchezo wake dhidi ya Intamba Murugamba ya Burundi 2-1 mjini Bujumbura.

Lesotho wanasonga mbele kwa kanuni ya magoli ya ugenini, baada ya kushinda mchezo wa awali 1-0 siku ya Ijumaa.

Mamba hao wa Lesotho sasa watapambana na Ghana, Zambia na Sudan katika kundi D la kufuzu.

Rwanda nayo ilitinga katika ngazi za makundi chini ya kocha mpya Milutin Sredojevic baada ya kuizaba Eritrea 3-1 kwenye mchezo wa pili uliochezwa kwenye uwanja wa Amahoro mjini Kigali.

Rwanda inaingia katika ngazi ya makundi kwa jumla ya magoli 4-2 baada ya kutoka sare na Eritrea mjini Asmara siku ya Ijumaa.

Sredojevic ambaye aliongoza Rwanda katika mchezo wake wa pili kufuatia kutimuliwa kwa kocha Sellas Tetteh, alizawadiwa magoli hayo na Olivier Karekezi, Jean Claude Iranzi na Labama Kamana.

Goli la Abraham Tedros katika dakika ya 90 halikuweza kusaidia lolote kwa Eritrea.

Equatorial Guinea nayo ilisonga mbele katika mazingira kama hayo, baada ya kupoteza mchezo wake 2-1 dhidi ya Madagascar mjini Antananarivo.

Wenyeji hao wa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika 2012 wamefuzu kwa kupata jumla ya mabao 3-2, kutokana na kushinda mchezo wa awali 2-0 siku ya Ijumaa.

Equatorial Guinea sasa itaungana na Tunisia, Cape Verde na Sierra Leone katika kundi B.

Kwa jumla Afrika itaandaa mechi 152 za kufuzu, ili kusaka timu tano ambazo zitacheza Kombe la Dunia 2014.

Timu hizo tano zitaiwakilisha Afrika katika fainali za Kombe la Dunia zitakazochezwa nchini Brazil kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1950.