Monday, September 22, 2014

BALLOTELLI APONZWA NA KEJELI ZAKE DHIDI YA MAN UTD MASHABIKI "WAMPA MAKAVU LIVE"

 
Mario Balloteli

Polisi nchini Uingereza wameanzisha uchunguzi kuhusu tukio ambalo mshambuliaji wa Liverpool kutoka Italia Mario Balotelli alitukanwa kutokana na rangi ya ngozi yake kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter.
Polisi katika mji wa Merseyside wameanzisha uchunguzi kufuatia matusi hayo yaliyotokea baada ya mshambulizi huyo wa Liverpool kutuma ujumbe akiicheka kichapo cha Manchester United mikononi mwa timu ndogo ya Leicester siku ya jumapili.
Baloteli aliandika ''Man Utd...LOL'' na ujumbe wake ukasambazwa zaidi ya mara 150,000 na mashabiki wake.

Hata hivyo miongoni mwa mwa wale waliouona ujumbe huo walimfokea kwa kuicheka United na wakamtusi kwa misingi ya rangi yake.
Japo ni raiya wa Italia Balotelli mwenye umri wa miaka 24 ana asili ya kiafrika.
Polisi tayari wamefunga kurasa kadha zilizotuma jumbe hizo huku wakianza uchunguzi waliozimiliki ni kina nani na wanaishi wapi iliwakamatwe na kujibu mashataka ya ubaguzi wa rangi.
Kundi linalopigania kumaliza ubaguzi wa rangi katika michezo Kick It Out lilisema kuwa baada ya kuarifiwa kuwepo kwa matusi yenye kumdhalilisha Balotelli, kundi hilo lilianzisha uchunguzi kwa ushirikiano na polisi wa mitandao ya kijamii.
Sio mara ya kwanza kwa Mshambulizi huyo kudhulumiwa kwa misingi ya rangi yake .
Balotelli ambaye alikuwa uwanjani Liverpool ilipolazwa 3-1 na West Ham jumamosi amewahi kudhulumiwa kwa misingi ya rangi yake timu ya Italia ilipokuwa ikijifua kwa kombe la dunia mwezi mei mwaka huu .
Awali pia aliwahi kutukanwa akiwa Inter Milan na pia akihudumu AC milan.