Thursday, February 7, 2013

MATOKEO MECHI ZA KIRAFIKI ZA KIMATAIFA

KIMATAIFA | MATOKEO


06 February
Honduras2 -  1   USA
06 February
Portugal2 - 3   Ecuador
06 February
France1 - 2   Germany
06 February
Republic of Ireland  2 - 0  Poland
06 February
Wales2 - 1   Austria
06 February
Belgium2 - 1   Slovakia
06 February
Scotland1 - 0   Estonia
06 February
Romania3 - 2    Australia
06 February
England2 - 1    Brazil
06 February
Greece0 - 0  Switzerland
06 February
Sweden2 - 3   Argentina
06 February
Netherlands1 - 1   Italy
06 February
Iceland0 - 2   Russia
06 February
Macedonia3 - 0  Denmark
06 February
Malta0 - 0  Northern Ireland
06 February
Turkey0 - 2  Czech Republic
06 February
Albania1 - 2    Georgia
06 February
Spain3 - 1   Uruguay
06 February
Israel2 - 1   Finland
06 February
Chile2 - 1    Egypt
06 February
Cyprus1 - 3   Serbia
 
06 February
Slovenia0 - 3   Bosnia-Herzegovina
06 February
Norway0 - 2  Ukraine
06 February
Hungary1 - 1  Belarus
06 February
Moldova1 - 3  Kazakhstan
06 February
Tanzania1 - 0  Cameroon
06 February
Azerbaijan1 - 0   Liechtenstein
06 February
Croatia4 - 0   Korea Republic
06 February
Rwanda2 - 2  Uganda
06 February
Kenya3 - 0   Libya
06 February
Zimbabwe2 - 1  Botswana
06 February
India2 - 4  Palestine
06 February
Japan3 - 0  Latvia
05 February
Luxembourg   1 - 1  Armenia
05 February
Senegal1 - 1  Guinea
02 February
Poland4 - 1   Romania

TANZANIA,UINGEREZA ZAFANYA KWELI ZAZIBANGUA CAMEROON NA BRAZIL

TAIFA Stars jana ilifanya kile kilichosubiriwa na mashabiki wa soka Tanzania baada ya kuitia ‘adabu’ Cameroon kwa kuichapa bao 1-0 katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa, shukrani kwa bao la ‘jioni’ kutoka kwa mshambuliaji wa kimataifa Mbwana Samata.

Samata anayecheza soka la kulipwa TP Mazembe ya DRC, alifunga bao hilo muhimu kwenye Uwanja wa Taifa dakika ya 89 baada ya kuusukumiza wavuni kirahisi mpira wa krosi ya Frank Domayo uliompita kipa wa Cameroon, Offala Komguep.

Bao la Samata lilikuja baada ya Stars inayoshika nafasi ya 124 kwa ubora wa viwango vya soka kufanya mashambulizi yasiyo na idadi lango kwa Cameroon.
Dakika 20 za mwisho wa kipindi cha kwanza, Cameroon haikuwa mchezo na badala yake jezi za rangi ya bluu ndizo zilizokuwa zikimili mpira.

Ni ushindi wa kwanza kwa Stars dhidi ya Cameroon, kwani matokeo mazuri waliyowahi kupata ni sare moja ya bila kufungana kwenye uwanja huohuo, na kisha kukubali kipigo cha mabao 2-1 nchini Cameroon.
Stars wangeweza kupata bao la kuongoza kipindi cha kwanza kama siyo beki Erasto Nyoni kushindwa kufunga penalti iliyochezwa na kipa.
Mechi hiyo ilianza taratibu na dakika 10 za kwanza zilionekana kama za wachezaji wa pande zote kusomana kimchezo.

Wenyeji Stars walitumia mfumo wa kushambulia pamoja na kukaba kwa pamoja kama alivyosema Kocha Poulsen kabla ya mchezo huo.
Cameroon, mabingwa wa zamani wa Mataifa ya Afrika, hawakuonekana kuwa wakali kama ambavyo mashabiki wengi waliojitokeza kushuhudia mchezo huo walitarajia.

Erasto Nyoni akijaribu kumtoka mlinzi wa Cameroon

Stars ikitumia mfumo wa 4-3-3, ilicheza vizuri kipindi cha kwanza, lakini hata hivyo Cameroon ndiyo walitawala mchezo, huku wakitumia mfumo wa 4-3-4.
Dakika ya 19, mpira ulisimama kwa muda baada ya kipa wa Stars Juma Kaseja kuumia kufuatia kugongana na Tchami Herve wa Cameroon.

Mabeki wa Stars,Aggrey Morris na Kelvin Yondan walifanya kazi ya ziada kuwazuia washambuliaji wa Cameroon sehemu kubwa ya kipindi cha kwanza.

Cameroon waliokuwa wakicheza bila nahodha Samuel Eto’o walikaribia kufunga bao katika dakika ya 24, baada ya Aboubakar Vincent kupiga kiki iliyotoka nje kidogo la lango la Stars. Nyoni angeweza kubadilisha ubao wa matokeo, kama siyo kushindwa kutumbukiza wavuni kiki ya penalti dakika ya 26 iliyotolewa na mwamuzi kutokana na Ngoula kuucheza mpira kwa mkono ndani ya eneo la hatari. Beki huyo wa Stars alikwenda kupiga penalti hiyo akionekana kutojiamini kabla ya shuti lake kupanguliwa na kipa Effala. Kipindi cha pili Stars ilicheza kwa nguvu na hapana shaka ndiyo walitawala sehemu kubwa, wakifanya mashambulizi mara kwa mara.Ngasa aliyeisumbua zaidi ngome ya Cameroon alimjaribu kwa shuti la mwendo mrefu kipa Offala ambaye alifanya kazi nzuri ya kulizuia.
Kiungo chipukizi Abubakary naye alikaribia kufunga kwa Stars kama siyo shuti lake kuchezwa na kipa wa cameroon ambaye sehemu kubwa ya kipindi cha pili hakupumzika kuokoa hatari
.
Pamoja na kufanya mabadiliko mengi kipindi cha pili, Stars waliendelea kutawala mchezo na kuwafunika Cameroon sehemu ya kiungo.

Katika mchezo huo, Stars ilifanya mabadiliko kwa kumtoa Mwinyi na kuingia Thomas Ulimwengu ambaye aliongeza nguvu ya mashambulizi.

Kipa wa Cameroon Efalla akiondosha hatari langoni mwake


Patashika kwenye lango la Cameroon

Mbwana Samatta akionesha udambwidambwi wake

Samattaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa goooooooooooollll

Mbwana Samatta akishangilia goli

Uingereza yaichapa Brazil
Katika mchezo mwingine uliochezwa huko duniani kati ya Uingereza na Brazil uliopigwa katika dimba la Wembley mashabiki wa soka wameshuhudia Uingereza ikiishushia kisago Brazil cha bao 2-1.
Goli la kwanza la Uingereza lilitupiwa kambani na Wayne Rooney baada ya kazi nzuri iliyofanywa na Jack Wilshere na Theo Walcott na mpira kumkuta Rooney nae bila ajizi akatupia kambani.
Katika mchezo huo Brazil walioonekana kuzidiwa sehemu ya katikati ambapo wachezaji kama Wilshere,Walcott na Cleverly walionekana kuwasumbua wabrazil sehemu ya katikati. na kuwafanya kina Ronaldhino Gaucho na Oscar kushindwa kufurukuta.

Ronaldhino alikosa penati katika mchezo huo iliyookolewa kitaalamu na kipa Joe Hart, Goli la kusawazisha la Brazil lilitupiwa kambani na Adriano kabla Frank Lampard hajatupia goli la pili na la ushindi kwa Uingereza.
Ronaldhino akicontrol mpira mbele ya Rooney


Rooney na wachezaji wenzake wakishangilia goli

Jack Wilshere akichanja mbuga

Mshikemshike Wilshere na Oscar 

Ronaldinho akijaribu kumalizia mpira wa penati uliiokolewa na Joe Hart bila mafanikio

Lampard akishangilia goli

Neymar chini ya ulinzi wa Gary Cahill

Mashabiki wa England
England 2-1 Brazil
 

MALI SI MALI KITU, YACHARAZWA 4-1 NA NIGERIA IKITINGA FAINALI

Nigeria yatinga fainali baada ya kuicharaza Mali magoli 4-1 katika mchezo wa kwanza wa nusu fainali za Kombe la Afrika.

Elderson Echiejile aliifungia Nigeria goli la kuongoza katika dk 24 na Ideye akaongeza msumari wa pili katika dk 29 ya mchezo.
Goli la tatu lilitupiwa kambani na Emenike katika dk 45 baada ya mpira alioupiga kumgonga Momo Sissoko wa Mali.

Hadi mapumziko Nigeria ilikuwa ikiongoza kwa 3-0.

Ahmed Musa alizidi kuleta majonzi kwa mashabiki wa Mali alipofunga bao la nne katika 59.

Mali ilizidi kusaka bao, katika dakika ya 74 Cheikh Diarra aliifungia timu yake bao la kufutia machozi.

Nigeria kuingia nusu fainali waliwabwaga Ivory Coast 2-1, timu ambayo ilikuwa inapewa nafasi kubwa ya kucheza fainali kutokana na ubora wa wachezaji wake.

Nayo Mali iliwatoa wenyeji wa mashindano Afrika Kusini kwa njia ya mikwaju ya penalti 3-1 baada ya timu hizo kucheza dakika 120 zikiwa zimefungana goli 1-1.

Timu nyingine katika nusu fainali za Afcon ni Ghana itakayokwaruzana na Burkina Faso. Ghana waliitoa Cape Verde katika hatua ya robo fainali kwa magoli 2-0, huku Burkina Faso wakiifunga Togo kwa goli 1-0.

Sasa Nigeria inamsubiri mshindi kati ya Ghana na Burkina Faso zinazocheza mchezo wa pili wa nusu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika 2013.

Wachezaji wa Nigeria wakimpongeza Emenike kwa kutupia bao maridadi sana

Tulia wewe sisi tumeahidiwa mademu alaah

Mlinda mlango wa Mali haamini kilichotokea


Hapa kazi tu kulala kwenuu

Mashabiki wa Nigeria wakilipuka kwa shangwe baada ya Nigeria kutinga fainali ya kombe la mataifa ya Afrika kwa kuibandua Mali 4-1
MALI 1-4 NIGERIA

BURKINA FASO YATINGA FAINALI YAIADHIRI GHANA

Burkina Faso, imetinga fainali baada ya kuilaza Ghana kwa njia ya mikwaju ya penalti baada ya timu hizo kutoka sare ya 1-1 katika dakika 120 za mchezo, ukiwa ni mchezo wa pili wa nusu fainali za kombe la mataifa ya Afrika.

Katika kipindi cha kwanza Ghana mnamo dk 12 walijipatia bao kwa mkwaju wa penati iliyopigwa na Wakasso. Bao hilo lilidumu mpaka mapumziko Ghana wakiwa kifua mbele,Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku kila timu ikitafuta bao na dk 59 bundi aliangukia katika lango la Ghana na mshambuliaji hatari A.Bance aliipatia Burkina Faso bao la kusawazisha na matokeo kuwa 1-1 katika dimba la Mbombela mchezo ukihudhuriwa na mashabiki 35,000.

Ghana ambao walikuwa wanapewa nafasi kubwa kucheza fainali, walishindwa kutamba mbele ya vijana wa Burkina Faso na kulazimika mikwaju ya penalti inatumika.

Ghana walipata penalti mbili tu, huku mbili zikipigwa nje na moja ikipanguliwa na mlinda mlango wa Burkina Faso.

Sasa Ghana itachuana na Mali kumtafuta mshindi wa tatu siku ya Jumamosi.

Jumapili, ndiyo siku yenyewe ya kujulikana bingwa. Je, ni Nigeria au Burkina Faso? Dakika 90 zitatoa jibu la kitendawili hicho.

A.Bance mfungaji wa goli la Burkinabe

Wakasso akiipatia goli Ghana kwa mkwaju wa penati mapema kabisa ya mchezo.

Mlinda mlango wa Burkinabe akiokoa hatari langoni mwake


Wachezaji wa Burkina Faso wakishangilia kutinga fainali baada ya mlinda mlango wao kupangua penati ya mwisho.

Mlinda mlango wa Burkina Faso

Asamoah Gyan Chini ya Ulinzi
Burkina Faso Vs Ghana penalty kickouts