Thursday, February 7, 2013

MALI SI MALI KITU, YACHARAZWA 4-1 NA NIGERIA IKITINGA FAINALI

Nigeria yatinga fainali baada ya kuicharaza Mali magoli 4-1 katika mchezo wa kwanza wa nusu fainali za Kombe la Afrika.

Elderson Echiejile aliifungia Nigeria goli la kuongoza katika dk 24 na Ideye akaongeza msumari wa pili katika dk 29 ya mchezo.
Goli la tatu lilitupiwa kambani na Emenike katika dk 45 baada ya mpira alioupiga kumgonga Momo Sissoko wa Mali.

Hadi mapumziko Nigeria ilikuwa ikiongoza kwa 3-0.

Ahmed Musa alizidi kuleta majonzi kwa mashabiki wa Mali alipofunga bao la nne katika 59.

Mali ilizidi kusaka bao, katika dakika ya 74 Cheikh Diarra aliifungia timu yake bao la kufutia machozi.

Nigeria kuingia nusu fainali waliwabwaga Ivory Coast 2-1, timu ambayo ilikuwa inapewa nafasi kubwa ya kucheza fainali kutokana na ubora wa wachezaji wake.

Nayo Mali iliwatoa wenyeji wa mashindano Afrika Kusini kwa njia ya mikwaju ya penalti 3-1 baada ya timu hizo kucheza dakika 120 zikiwa zimefungana goli 1-1.

Timu nyingine katika nusu fainali za Afcon ni Ghana itakayokwaruzana na Burkina Faso. Ghana waliitoa Cape Verde katika hatua ya robo fainali kwa magoli 2-0, huku Burkina Faso wakiifunga Togo kwa goli 1-0.

Sasa Nigeria inamsubiri mshindi kati ya Ghana na Burkina Faso zinazocheza mchezo wa pili wa nusu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika 2013.

Wachezaji wa Nigeria wakimpongeza Emenike kwa kutupia bao maridadi sana

Tulia wewe sisi tumeahidiwa mademu alaah

Mlinda mlango wa Mali haamini kilichotokea


Hapa kazi tu kulala kwenuu

Mashabiki wa Nigeria wakilipuka kwa shangwe baada ya Nigeria kutinga fainali ya kombe la mataifa ya Afrika kwa kuibandua Mali 4-1
MALI 1-4 NIGERIA

No comments:

Post a Comment