Wednesday, January 16, 2013

HAPPY BIRTHDAY KHALED VAN GOMEKA KATULUMULA

Leo ni siku yangu ya kuzaliwa, Mnamo tarehe 16.1.1979 Mwanaidi Salum Ntandu ambae kwasasa ni marehemu, mungu amsamehe dhambi zake,amuepushie adhabu ya kaburi na ailaze roho yake mahali pema peponi,Amin. Alijifungua mtoto wa kiume majira ya usiku na kwa Upendo yeye pamoja na Mume wake Mpenzi wakampa mtoto wao jina la Shida. Yaliyowasibu mpaka kumpa mtoto wao jina hilo mimi na wewe hatujui.

Shida alipofikia umri wa miaka 5 alibatizwa na akapewa jina la Goefrey Jonathan. Miaka kadhaa Marehemu Mwanaidi Salum(mama wa mtoto) na Jonathan Katulumula(baba wa mtoto) wakafikia makubaliano ya mume kubadilisha dini na kufuata dini ya mkewe na sasa mzee Jonathan akawa anajulikana kama Jaffary, kutokana na mabadiliko hayo mtoto wao Geofrey Jonathan alikuwa darasa la 6 nae alibadilishwa jina,Namzungumzia Kijana mtanashati, mwenye upendo na asiependa makuu KHALID JAFFARY GOMEKA (KHALED VAN GOMEKA). ambae leo ndio siku yake ya kuzaliwa kwa kidhungu BIRTHDAY

KHALID J GOMEKA (Van Gomeka)
“This is a special day not just because it is my birthday, but also because I see your greetings and I feel fortunate to have friends. Thank you.”