Friday, November 18, 2011

WAMAREKANI WAANDAMANA KUPINGA TOFAUTI KUBWA KATI YA TAJIRI NA MASIKINI

Waandamanaji wanaopinga tabaka la masikini na matajiri wakiwa katika mtaa mdogo wa Manhattan karibu na soko kuu la hisa "New York stock exchange" katika siku waliyoiita siku ya vitendo wakiwa wameandamana kutoka New york mpaka New York stock exchange

Maelfu ya waandamanaji katika mji wa New York wameendelea na harakati zao wakielekea kuvuka daraja la Brooklyn, kuonyesha ghadhabu zao dhidi ya kuendelea kuwepo matabaka nchini humo.


Waandamanaji wanaadhimisha kuanza kwa kampeni ya kupinga mfumo wa kiuchumi unaosababisha matabaka nchini Marekani ambapo walipiga kambi katika mtaa wa Wall Street kuliko na soko kuu la hisa na taasisi kubwa za kifedha Marekani. Mwezi uliopita, polisi waliwakamata mamia ya waandamaji .

Taswira nje ya soko kuu la fedha la Marekani ni raia wenye ghathabu kubwa wakiendelea kukaribia jumba la soko hilo na kulizingira kabisa.Polisi wamekuwa na wakati mgumu kuwazuia kwa kuweka vizuizi nje ya jumba hilo. Baadhi ya waandamanaji wamekamatwa huku kukiwa na makabiliano na ujibizanaji wa maneno makali.


Waandamanaji wakiwa wamebeba bango

Hamasa ya waandamanaji hao ni kufuatia hatua ya polisi kuwafurusha katika eneo walikokita kambi katika bustani ya Zuccotti. Hii imewafanya kushindwa kukesha huko. umati wa watu ambao walikuwa wamekusanyika nje ya Wall Street wameondoka.

Backed for the first time in large numbers by US trade unions, ‘Occupy Wall Street’ protesters pour into New York’s financial district. REUTERS photo

Hata hivyo wamepanga kukusanyika tena katika kituo cha treni na jioni watafanya jaribio jingine la kuvuka daraja kuu ya Brooklyne.
Waandamanji hao wanasisitiza kwamba ni haki yao kuandamana.