Tuesday, July 5, 2011

TAKUKURU NI "JOKA LA KIBISA"

Watanzania wengi tuliposikia kuwa serikali imeanzisha taasisi ya kupambana na kuzuia rushwa (TAKUKURU) tulifarijika sana na tukajua wazi kuwa sasa wale ambao walikuwa wanakula jasho letu na kulitia hasara taifa kwa mikataba feki,matumizi hewa na ujanja ujanja mwingine wakati wao umefika. Hali imekuwa tofauti na matarajio ya wengi kwani chombo hicho nyeti kimeonesha mapungufu makubwa kama sio madhaifu, Kwa mujibu wa tafiti zilizofanywa zimegundua chombo hiki kuwa na udhaifu mkubwa katika kusimamia kesi na utekelezaji wa kazi zake,imebainika kuwa TAKUKURU imeshinda kesi moja tu na 99% ya kesi imeshindwa na kusababisha hasara ya kuwalipa walioshinda kesi fidia na malimbikizo ya mishahara, Katika hili Taifa linaendelea kupata hasara kutokana na TAKUKURU kutowajibika ipasavyo na inanipelekea kuona sasa chombo hiki hakina tofauti na nyoka wa Kibisa ambaye hana madhara pindi anapokuwa nacheza na binadamu.Naomba serikali itazame upya jinsi ya kuendesha chombo hiki nyeti katika Taifa.