Monday, April 30, 2012

SIMBA S.C.....WE ACHA 2!! YAIBANJUA AL AHLY SHANDY 3-0



Timu ya Simba maarufu kama watoto wa Msimbazi ya jijini Dar es Salaam wameendeleza kipigo dhidi ya timu za kigeni safari hii timu ya Al Ahly Shandy ya Sudan imepata kichapo kingine kwa kubanjuliwa mabao 3-0 katika mpambano mkali wa kuvutia uliojaza wapenzi wa soka uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam kwenye mechi ya kuwania ubingwa wa kombe la shirikisho la  klabu za Afrika.
Emmanuel Okwi akijaribu kuipenya ngome ya Al Ahly Shandy ya Sudan

Umati wa mashabiki wa soka waliohudhuria walilipuka kwa shangwe pale mshambiliaji Haruna Moshi"Boban" alipotupia kambani  balo la kwanza baada ya kazi nzuri iliyofanywa na mshambuliaji mwenzake Uhuru selamani.
Bao la pili lilifungwa na mshambuliaji Patrick Mafisango"Mutesa" ambaye alikosesha timu yake bao kwa njia ya penati baada ya kupiga mpira penati mbofumbofu iliyodakwa na Mlinda Mlango wa Al Ahly Shandy.
Wachezaji wa Simba wakishangilia bao la pili lililofungwa na Mafisango

Bao safi lililofungwa na Mshambulaiji kutoka Uganda, Emmanuel Okwi liliwainua watazamaji wote uwanjani kwani bao hilo lilikuwa la kifundi sana na kuifanya timu ya Simba kuibuka kifua mbele kwa mabao 3-0 dhidi ya Al Ahly Shandy ya Sudan.
Mabao yote yalifungwa katika kipindi pili cha mchezo huo ambao ulijaa shauku kubwa kutoka kwa wanachama wa timu ya simba ambayo imeingia 16 bora katika kombe la shirikisho la klabu za Afrika.
Kocha wa Simba Milovan akishangilia pamoja na wachezaji wake
Umati wa Mashabiki wa Simba wakishangilia kwa mbwembwe


Simba na Al Ahly Shandy ya Sudan zitachauana tena Mei 11 mwaka huu katika mchezo wa marudiano wa michuano ya kombe la shirikisho la klabu za Afrika.