Monday, August 12, 2013

MAN U YATWAA NGAO YA HISANI, MOYES AUANZA MSIMU VYEMA

Timu ya soka ya Manchester United ya Uingereza imetwaa ngao ya hisani ikiwa ni ishara ya ufunguzi mwema wa msimu huu kwa kuitandika timu ya Wigan kwa bakora 2-0 katika dimba la Wembley.
Ushindi huo ni wa kwanza kwa kocha mpya wa Man U Moyes ambaye amepokea mikoba ya aliekuwa kocha wa Man U kwa miaka mingi Sir Alex Furguson , na hii ni kiashirio kizuri kwa Moyes.
Katika mpambano huo wa Ngao ya hisani sio mwingine alieipatia ushindi Man U bali ni ile ile LULU waliyoiokota Emirates,Robin Van Persie aliepachika mabao yote mawili katika mpambano huo.
 
Umati wa mashabiki ukielekea katika dimba la Wembley kushuhudia mpambano wa ngao ya hisani kati ya Man UNITED na Wigan Athletics.
 
Man U 2-0 wIGAN

Van Persie akipiga kichwa kutupia bao la kwanza la Man United.
 
Van Persie akijaribu kuwatoka walinzi wa Wigan Athletic

Van Persie na wenzake wakishangilia goli

Kocha wa Man United David Moyes akifurahia ngao ya hisani

Robin Van Persie akiwa na furaha tele baada ya kuiwezesha Man U kutwaa ngao ya hisani