Thursday, July 5, 2012
HASHEEM THABEET AULA OKC KUVUNA DOLA 880,000
Hasheem akifanya majamboooozz!!!
Nyota wa kikapu Mtanzania Hasheem Thabeet ameula baada ya kupata dili murua la kuhamia timu ya mpira wa Kikapu ya Oklahoma City Thunder (OKC) akitokea Portland Trail blazers ambapo kabla ya Portland alitokea Memphis Zote za nchini Marekani.
Habari zinasema Hasheem amesaini mkataba wa 'nyundo' mbili na anatarajiwa kuvuna umatemate wa kiasi cha dola za kimarekani 880,000 kwa mwaka a.k.a Nyundo.
Haya sasa vijana waliopo katika mchezo wa kikapu fuateni nyayo hizo.
Basketball sio lelemama lazima uwe umeshiba
Hasheem akiwa na rais wa Tanzania Mh Jakaya Mrisho Kikwete alipotembelea Ikulu jijini Dar es salaam
Menu time!!!!
YANGA YATIMULIWA ZANZIBAR KOCHA MPYA ATINGA DAR
Kocha mpya wa Yanga Tom Saintfiet alipowasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwl J.K Nyerere,Dar es salaam.
KOCHA mpya wa Yanga, Tom Saintfiet (39) ametua nchini jana mchana, akitanguliza kauli kwamba, atatumia uzoefu wake kimataifa katika taaluma ya ukocha kuleta mageuzi makubwa ndani klabu hiyo ya Jangwani.Saintfiet, raia wa Ubelgiji alitua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere na kulakiwa na mamia ya mashabiki wa Yanga wakiongozwa na Katibu Mkuu, Celestine Mwesingwa.
Akizungumzia ujio wake, Saintfiet atakayerithi mikoba ya Kostadin Papic, alisema anaifahamu Yanga muda mrefu baada ya kuifuatilia katika mitandao pamoja na mashindano ya Kagame.
"Mimi siyo mgeni na Soka la Afrika, nalifahamu vizuri nimefanya kazi Nigeria, Zimbabwe, Namibia na Ethiopia. Kwa sababu hiyo, sioni kikwazo cha kushindwa kufikia malengo yangu.
"Isitoshe habari za Yanga na soka la Afrika Mashariki nazifahamu kupitia kusoma kwenye tovuti mbalimbali.
"Mwaka jana nilifuatilia kupitia kituo cha Super Sport kilichokuwa kinarusha mashindano ya Kagame," alisema Saintfiet.
"Zaidi natarajia kupata ushirikiano wa kutosha kutoka kwa uongozi na mashabiki ili kazi yangu iwe rahisi kuitekeleza."
Baada ya kuzungumza na wanahabari, Saintfiet alipanda katika gari aina ya Land Cruiser mpaka makao makuu ya klabu akisindikizwa na msafara wa mabasi madogo matatu.
Makao makuu, Mtaa wa Jangwani, Saintfiet alifanya mazungumzo mafupi na Mwesigwa kisha akaelekea kwenye ukumbi na kuwasalimu mamia ya mashabiki waliokuwapo kumlaki.
"Nashukuru kwa mapokezi mazuri mliyonipa, kilichobaki ni kufanya kazi iliyonileta ili Yanga iweze kufikia mafanikio," alisema Saint Fiet.
Kwa mujibu wa msemaji wa Yanga Louis Sendeu, leo asubuhi Saintfiet atakutana na uongozi wa Yanga kwa mazungumzo kabla ya kusaini mkataba.
Wakati huohuo, habari zilizolifikia Mwananchi jana jioni zilidai kuwa Yanga imeondolewa katika michuano
ya Kombe la Urafiki inayoendelea mjini Zanzibar baada ya kukiuka masharti ya waandaaji.
"Tumeiondoa Yanga katika mashindano yetu ya Urafiki kutokana na kwenda kinyume na maelekezo ya barua ya mwaliko.
Tuliwataka kuleta timu itakayocheza michuano ya Kombe la Kagame, lakini wamefanya kinyume chake kwa kuleta timu B.
"Wametusababishia hasara kubwa, mashabiki wamekasirishwa, hawana tena hamu ya kuja uwanjani," alisema msemaji wa Chama cha Soka Zanzibar (ZFA), Munir Zakaria.
Walipoulizwa viongozi wa Yanga hawakuwa tayari kusema lolote kwa madai kuwa walikuwa na jukumu kubwa la mapokezi ya kocha wao mpya.
Katika hatua nyingie, Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) jana ilitoa kiasi cha Sh20 milioni kwa ajili ya kufanikisha maandalizi ya Uchaguzi Mdogo kuziba nafasi zilizoacha wazi kufuatia uongozi wa awali kujiuzulu.
Uchaguzi huo umepangwa kufanyika jijini Dar es Salaam Julai 14 kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee.
Akikabidhi hundi jana, Meneja wa Bia ya Kilimanjaro George Kavishe alisema pesa hizo ni sehemu ya udhamini wa TBL kwa Yanga.WASIFU WA KOCHA MPYA YANGAKuzaliwa:
29-3-1973
Timu za Taifa:
Namibia,
Ethiopia,
Zimbabwe
Qatal
Klabu:
Al Gharafa (Qatal)
Rops(Finland),
B71 (Visiwa vya Island)
BV Cloppenburg ya Ujerumani.
Umati wa mashabiki wa Yanga waliofika Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwl JK Nyerere kumlaki kocha wao mpya Tom Saintfiet
Kocha mpya wa Yanga kutoka Ubelgiji Tom Saintfiet akizungumza na mapaparazzi katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwl JK Nyerere jijini Dar es salaam.
Subscribe to:
Posts (Atom)