Zdravko Logarusic raia wa Croatia.
Baada ya kuwatimua makocha wake, Abdallah Kibadeni na msaidizi wake,
Jamhuri Kiwhelo ‘Julio’, Simba sasa imemchukua kocha Zdravko Logarusic
raia wa Croatia.
Tayari Simba imemaliza mazungumza na kocha huyo na anatarajia kutua
nchini hivi karibuni kwa ajili ya kusaini mkataba na mara moja kuanza
kazi.Kabla ya hapo, Logarusic alikuwa kocha wa Gor Mahia ya Kenya
aliyoifundisha kwa misimu miwili akisha nafasi ya pili.Msimu huu ulikuwa
wa mwisho kabla ya kubwaga manyanga na kumuachia mikoba Bobby Willismson , ambaye kulikuwa na uvumi kwamba angekuja kuitumikia Simba S.C.