Wednesday, April 30, 2014

RONALDO AVUNJA REKODI YA KUTUPIA UEFA

 

CHRISTIANO RONALDO

Nyota wa Real Madrid ya Uhispania Cristiano Ronaldo amevunja rekodi ya Lionel Messi ya ufungaji mabao mengi zaidi katika ligi ya mabingwa barani Uropa alipoifungia timu yake mabao mawili na kuisaidia

kuichapa Bayern Munich mabao 4-0 katika nusu fainali jana usiku.

Mreno huyo mwenye umri wa miaka , 29,alifunga bao lake la 15 na 16 msimu huu katika uwanja wa Allianz Arena.

Kufuatia ushindi huo Real Madrid ilifuzu kwa fainali ya mchuano huo kwa jumla ya mabao 5-0.

Ronaldo sasa amefunga mabao 16 katika mechi kumi za ligi hiyo ya mabingwa Barani Ulaya mbili zaidi ya Lionel Messi wa Barcelona .

Rekodi hiyo ya mabao 14 ilikuwa ikishikiliwa kwa pamoja kati ya Messi (2011-12, Barcelona), Ruud van Nistelrooy (2002-03, Manchester United) na Jose Altafini (1962-63, AC Milan).

Kwa jumla Ronaldo amefunga mabao 67 katika ligi hiyo ya mabingwa barani ulaya sawa na Messi na ni mabao manne tu nyuma ya rekodi ya idadio kubwa zaidi ya mabao yaliyofungwa na mchezaji wa zamani wa Real na Schalke Raul.

 

REAL MADRID YABOMOA UKUTA WA BERLIN, YATINGA FAINALI UEFA

Vigogo wa ligi kuu ya Uhispania Real Madrid, wamekuwa timu ya kwanza kufuzu kwa fainali ya ligi ya mabingwa barani ulaya baada ya kuinyeshea Mabingwa watetezi wa kombe hilo Bayern Munich ya Ujerumani kwa mabao manne kwa nunge na hivyo kuibuka a ushindi mkubwa wa jumla ya mabao 5-0.

Sergio Ramos alifunga mabao mawili mapema katika kipindi cha kwanza cha mechi hiyo.

  

Ramos akitupia kambani goli la kwanza

Kabla ya nyota wa Ureno na mchezaji bora duniani Christiano Ronaldo kuihakikishia Madrid fainali yao ya kwanza tangu mwaka wa 2002 na mkwaju wa wa freekick.

Bao hilo lilikuwa lake la 16 katika ligi ya mabingwa barani Uropa.

Kwa Bayern, kichapo hicho kilikuwa ni kama wembe wa kutu kwao kwani mwaka uliopita Wajerumani hao waliifunga Barcelona 7-0 katika hatua ya nusu fainali kabla ya kuilaza Borussia Dortmund na kutwaa taji lao la tano barani ulaya.

Haijulikani kufikia sasa iwapo halmashauri inayoingoza klabu hiyo itachukua hatua yeyote dhidi ya kocha wa klabu hicho Pep Guardiola ambaye licha ya kuiongoza Barca kutwaa taji la Bundesliga ameshindwa kutetea hadhi ya klabu hiyo katika mchuano huu wenye kitita kikubwa zaidi.

 

Nimeuaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa

 

Oyooooooo...Sergio Ramos akishangilia goli

Madrid sasa inasubiri kujua iwapo itachuana na Chelsea ya Uingereza chini ya ukufunzi wake aliyekuwa kocha wao Jose mourinho ama wapinzani wao wa mji wa Madrid , Athletico .

Mshambulizi wa Athletico Madrid Diego Costa alisema anatumai Chelsea hawata regesha basi kwenye lango lao ilhali watacheza mchezo yenye maarifa.

Timu hizo zilitoka sare tasa katika mkondo wa kwanza .

  

 

 

 

 
BAYERN MUNICH 0-4 REAL MADRID