Friday, May 27, 2011

KITABU KIKUBWA KULIKO VYOTE DUNIANI

Pichani ni kitabu kinachoaminika kuwa ni kitabu kikubwa kiliko vyote duniani kikiwa na kurasa milioni 1.5 ingawaje chanzo cha habari hakikuthibitisha hilo.

DJ BOO KUWARUSHA WASHIRIKI BIG BROTHER JUMAMOSI HII.


Jumamosi hii washiriki waliomo katika jumba la Bigbrother Afrika watapata nafasi ya kuruka majoka ambapo katika moja na mbili atakuwepo Dj mashuhuri kutokaFM 101 Chifundo Ntwana a.k.a DJ BOO.Katika pati hilo lijulikanalo kama The 411 Party Catch.
Katika hali isiyo ya kawaida mshiriki mmoja aliyemo ndani ya jumba hilo wakati wa mazoezi aliwaonesha washiriki wenzake sinema ya bure kwa kuacha shanga za kiuno nje kwa hapa nyumbani maarufu kama "chachandu". wakati wenzake hasa wa jinsia tofauti wakikodolea macho yeye hakuonesha kujali na kuendelea kuchange mosheni vile awezavyo.

WASEMAVYO WACHEZAJI JUU YA MECHI DHIDI YAO KATI YA BARCA NA MAN U.

Patrice Evra mchezaji hodari wa Man United amefunguka na kusema kuwa hatakiwi kupoteza fainali nyingine ya ligi ya mabingwa ya ulaya. "Kama nimecheza fainali nne na kushinda moja tu itakuwa ngumu kuendelea kucheza fainali za ligi ya mabingwa na labda nimuambie kocha asinichezeshe tena katika fainali" alisema Evra. aliendelea kusema,"ni muhimu kushinda fainali hii na ni muhimu kuiweka Man United kileleni mwa ulimwengu wa soka"
Evra mwenye miaka 30 ameshaipatia Man United rekodi ya kuchukua mataji ya ndani mara 19. "kombe la mabingwa ni ushindi mnono ambao kila mtu anataka kuutwaa na usiku wa fainali ya mabingwa ni maajabu na ninapata hisia pale tuliposhinda lakini kushindwa ni hisia mbaya sana na sitaki zitokee tena" alisema Evra.

Javier Mascherano amefunguka na kusema kuwa hatojisikia vibaya akikosekana katika kikosi cha kwanza cha Barcelona katika fainali hiyo dhidi ya Man United kwani kwake kuwepo katika kikosi cha Barcelona ni heshima kubwa. "wachezaji wakubwa na timu kubwa ni hapa nilipo na ninajisikia vizuri kuwa sehemu ya kikosi" alisema Mascherano.

Kiungo wa Man United Michael Carrick nae amefunguka na kusema kuwa yupo fiti na tayari kuwazodoa wale wote ambao wanabeza kiwango chake kwa sasa.mashabiki wamekuwa hawana imani nae.

MAN UNITED vs F.C BARCELONA

Hayawi hayawi sasa yamekuwa ule mpambano wa kukata na mundu wa fainali ya mabingwa barani ulaya "uropa" kati ya Manchester United ya uingereza dhidi ya Football Club Barcelona ya Hispania utapigwa kesho katika dimba la Wembley nchini Uingereza. Hii inaashiria kuisha kwa majigambo ya kipindi kirefu baina ya mashabiki wa Timu hizo mbili zenye kupendwa zaidi barani ulaya na sehemu nyingine za dunia na siku hiyo sio nyingine bali ni siku ya kesho tarehe 28 mwezi wa 5 mwaka huu mzuri wa 2011. Ngoja tusubiri ni masaa kadhaa tu yamesalia kuanza kwa kipute hicho ambapo kwa taarifa nilizozipata ni kwamba pweza ameitabiria ushindi Man united,huo ni utabiri tu wahenga walisema maneno matupu hayavunji mfupa
 Nembo ya timu ya mpira wa miguu ya Football Club Barcelona ya Hispania.
Nembo ya chama cha soka cha ulaya.

 Mshambuliaji wa Timu ya Manchester United Wayne Rooney ambaye anategemewa kuongoza safu ya mashambulizi hapo kesho watakapokutana na F.C. Barcelona katika fainali ya ligi ya mabingwa wa ulaya katika dimba la Wembley jijini London nchini Uingereza.
Leonel Messi mshambuliaji machachari wa F.C. Barcelona ambaye anategemewa kuwa mwiba wenye sumu kali dhidi ya Manchester United hapo kesho katika fainali hiyo ya ligi ya mabingwa barani ulaya.
Nembo ya Timu ya Manchester United ya uingereza.