Friday, May 27, 2011

MAN UNITED vs F.C BARCELONA

Hayawi hayawi sasa yamekuwa ule mpambano wa kukata na mundu wa fainali ya mabingwa barani ulaya "uropa" kati ya Manchester United ya uingereza dhidi ya Football Club Barcelona ya Hispania utapigwa kesho katika dimba la Wembley nchini Uingereza. Hii inaashiria kuisha kwa majigambo ya kipindi kirefu baina ya mashabiki wa Timu hizo mbili zenye kupendwa zaidi barani ulaya na sehemu nyingine za dunia na siku hiyo sio nyingine bali ni siku ya kesho tarehe 28 mwezi wa 5 mwaka huu mzuri wa 2011. Ngoja tusubiri ni masaa kadhaa tu yamesalia kuanza kwa kipute hicho ambapo kwa taarifa nilizozipata ni kwamba pweza ameitabiria ushindi Man united,huo ni utabiri tu wahenga walisema maneno matupu hayavunji mfupa
 Nembo ya timu ya mpira wa miguu ya Football Club Barcelona ya Hispania.
Nembo ya chama cha soka cha ulaya.

 Mshambuliaji wa Timu ya Manchester United Wayne Rooney ambaye anategemewa kuongoza safu ya mashambulizi hapo kesho watakapokutana na F.C. Barcelona katika fainali ya ligi ya mabingwa wa ulaya katika dimba la Wembley jijini London nchini Uingereza.
Leonel Messi mshambuliaji machachari wa F.C. Barcelona ambaye anategemewa kuwa mwiba wenye sumu kali dhidi ya Manchester United hapo kesho katika fainali hiyo ya ligi ya mabingwa barani ulaya.
Nembo ya Timu ya Manchester United ya uingereza.

No comments:

Post a Comment