Thursday, May 26, 2011

WANAFUNZI WENYE HASIRA WACHOMA MOTO SHULE.

                                                                     Sehemu ya mabaki ya shule hiyo baada ya huchomwa moto.
Wanafunzi wa shule ya secondary ya Amadeski Ashile Esikoleni i Sizinda ya Kwazulu Natal nchini Africa ya kusini wamechoma moto madarasa matatu ya shule hiyo kwa kile kilichoelezwa kutokuridhishwa na uongozi wa shule hiyo. Msemaji wa idara ya elimu ya Kwazulu Natal Sihle Mlotshwa ameelezea kusikitishwa na kitendo hicho,pia kamanda wa polisi wa Kwazulu amesema hakuna aliyekamatwa kutokana na tukio hilo na hakuna aliyejeruhiwa na hasara iliyosababishwa na fujo hizo haikuweza kujulikana mara moja.

No comments:

Post a Comment