Friday, May 27, 2011

WASEMAVYO WACHEZAJI JUU YA MECHI DHIDI YAO KATI YA BARCA NA MAN U.

Patrice Evra mchezaji hodari wa Man United amefunguka na kusema kuwa hatakiwi kupoteza fainali nyingine ya ligi ya mabingwa ya ulaya. "Kama nimecheza fainali nne na kushinda moja tu itakuwa ngumu kuendelea kucheza fainali za ligi ya mabingwa na labda nimuambie kocha asinichezeshe tena katika fainali" alisema Evra. aliendelea kusema,"ni muhimu kushinda fainali hii na ni muhimu kuiweka Man United kileleni mwa ulimwengu wa soka"
Evra mwenye miaka 30 ameshaipatia Man United rekodi ya kuchukua mataji ya ndani mara 19. "kombe la mabingwa ni ushindi mnono ambao kila mtu anataka kuutwaa na usiku wa fainali ya mabingwa ni maajabu na ninapata hisia pale tuliposhinda lakini kushindwa ni hisia mbaya sana na sitaki zitokee tena" alisema Evra.

Javier Mascherano amefunguka na kusema kuwa hatojisikia vibaya akikosekana katika kikosi cha kwanza cha Barcelona katika fainali hiyo dhidi ya Man United kwani kwake kuwepo katika kikosi cha Barcelona ni heshima kubwa. "wachezaji wakubwa na timu kubwa ni hapa nilipo na ninajisikia vizuri kuwa sehemu ya kikosi" alisema Mascherano.

Kiungo wa Man United Michael Carrick nae amefunguka na kusema kuwa yupo fiti na tayari kuwazodoa wale wote ambao wanabeza kiwango chake kwa sasa.mashabiki wamekuwa hawana imani nae.

No comments:

Post a Comment