
Ligi ya mabingwa barani ulaya imeendelea tena hapo jana huku wapenda soka ulimwenguni wakishuhudia Vijana wa Mourinho Chelsea wakitandikwa na FC Basel palepale darajani kwa bao 2-1.
Huku nako ikishuhudiwa timu mbili zenye soka safi na la kuridhisha yaani FC Barcelona ya Uhispania na Arsenal ya Uingereza zikifanya mauaji, Barcelona wakiiadabisha Ajax ya Uholanzi nayo Arsenal ikiitandika Marseille ya Ufaransa.

Oscar akishangilia goli la kwanza la Chelsea
Marco Streller akishangilia goli lililoizamisha Chelsea darajani
Wachezaji wa FC Basle wakishangilia ushindi dhidi ya Chelsea
CHELSEA 1-2 FC BASLE
Katika mpambano kati ya Chelsea waliokuwa wenyeji wa mchezo huo pale darajani mabao ya timu zote mbili yalitupiwa kambani na Oscar (44) na yale ya Basle yalitupiwa kambani na M Salah (70) na Steller (81).
Katika mtanange baina ya Arsenal na Marseille mabao yalitupiwa kambani na Walcott (64) na Ramsey (83) na la kufutia machozi lilitupiwa kambani kwa mkwaju wa penati na Jordan Ayew (90).
Theo Walcott Walcott akitupia kambani bao la kwanza

Walcott akishangilia
Ramsey akishangilia baada ya kutupia kambani bao la pili

Giroud na Ozil wakimpongeza Ramsey

Ozil kibaruani
MARSEILLE 1-2 ARSENAL
Barcelona na Ajax mabao yalitupiwa kambani na Leonel Messi (21,54 na 74) na Pique (68).
Messi akifanya mauaji

Zuia hiyooooooooooooooooooooooo

Messi akipiga faulo iliyoenda moja kwa zote kambani

Iniesta akifanya udambwidambwi

Messi akitoka na mpira wake baada ya kutupia kambani mabao matatu ''Hat Trick''
BARCELONA 4-0 AJAX
Matokeo ya mechi zote
AC Milan 2-0 Celtic
Chelsea 1-2 FC Basle Marseille 1-2 Arsenal Atletico Madrid 3-1 Zenit St Petersburg Austria Vienna 0-1 Porto Barcelona 4-0 Ajax Napoli 2-1 Borussia Dortmund Schalke 04 3-0 Steaua Bucharest |
No comments:
Post a Comment