Wednesday, December 19, 2012

KUUNGANISHA UMEME SASA BEI CHEE

SHIRIKA la Umeme Tanzania (Tanesco), limetangaza rasmi kupunguza viwango vya kuunganisha umeme kuanzia Januari Mosi, 2013 ikiwa ni utekelezaji wa ahadi ya Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo aliyoitoa katika Bunge la Bajeti lililopita.

Meneja Mawasiliano wa Tanesco, Badra Masoud amesema kupunguzwa kwa viwango hivyo kutasaidia wananchi wengi kuunganisha umeme.
Badra alisema gharama za kuunganisha umeme vijijini katika umbali usiozidi mita 30 bila nguzo sasa itakuwa Sh177,000 na wateja wa mijini watatakiwa kulipia Sh320,000 badala ya Sh455,108 za sasa akisema punguzo hilo ni sawa na asilimia 61.11 kwa wateja waishio vijijini na asilimia 29.48 kwa wateja wa mijini.

Alisema kwa wateja wanaoishi vijijini wanaohitaji umeme wa njia moja na nguzo moja watatakiwa kulipia Sh337,740 wakati wale wa mijini watalipia Sh515,618 badala ya Sh1,351,884 zinazolipwa na wateja hivi sasa.

“Punguzo hilo ni sawa na asilimia 75.02 kwa wateja waishio vijijini na asilimia 61.86 kwa wateja waishio mijini.”

Alisema wateja wa vijijini watakaojengewa njia moja na nguzo mbili watatakiwa kulipia Sh454,654 na wa mijini watalipia Sh696,670, badala ya Sh2,001,422 ambazo zinalipiwa hivi sasa.Alisema punguzo hilo ni sawa na asilimia 77.28 kwa wateja waishio vijijini na asilimia 65.19 kwa wateja wa mijini.

Meneja mawasiliano wa Tanesco,Badra Masoud akifafanua jambo.
 

No comments:

Post a Comment