Thursday, July 21, 2011

JAPAN MABINGWA WA DUNIA SOKA LA WANAWAKE

Japan imeilaza Marekani kwa mikwaju ya penalti 3-1 na kuwa nchi ya kwanza kutoka bara Asia kushinda Kombe la Dunia kwa wanawake.
Wachezaji wa Japan Wakishangilia ubingwa wa dunia kwa wanawake

Saki Kumagai ndiye aliyefunga mkwaju wa penalti wa ushindi baada ya mlinda mlango wa Japan, Ayumi Kaihori kuokoa mikwaju mwili ya penalti kati ya mitatu ya wanadada wa Marekani.
Alex Morgan alikuwa wa kwanza kuifungia Marekani bao, kabla ya Aya Miyama kusawazisha dakika za mwisho za muda wa kawaida.
Abby Wambach aliipatia Marekani bao la pili katika muda wa nyongeza, lakini Homare Sawa alihakikisha kutakuwa na kandanda ya kusisimua ya fainali baada ya kusawazisha zikiwa zimesalia dakika nne mchezo kumalizika, alipounganisha mpira wa kona ulioingia moja kwa moja wavuni.
Marekani watajilaumu wenyewe kwa kushindwa kuweka rekodi ya kunyakua Kombe la dunia kwa mara ya tatu, baada ya kumiliki mchezo kwa kipindi kirefu. Lakini pia wanadada hao wa Marekani walishindwa kutumia vyema nafasi walizopata kufunga mabao hasa kipindi cha kwanza.
Wambach mshambuliaji wa Marekani alikuwa tishio kwa ngome ya Japan na alikaribia kufunga wakati mkwaju wake kugonga mwamba na kutoka nje.
Japan, ambao walikuwa hawajawahi kuishinda Marekani katika michezo 25 waliyokutana siku za nyuma, ambapo walifungwa mara 22, walionekana kuwazidi wapinzani wao katika mashambulio ya kushtukiza. Mbinu hiyo ya kushambulia kwa kushtukiza iliwasaidia sana walipocheza na wenyeji Ujerumani katika hatua ya robo fainali na vile vile walipoitoa Sweden hatua ya nusu fainali, lakini ngome ya Marekani ilikuwa ikikabiliana na wanadada hatari wa Japan, Nahomi Kawasumi na Kozue Ando ambao kwa kiasi fulani walifanikiwa kuwatia mfukoni.

No comments:

Post a Comment