Monday, May 23, 2011

BARCELONA YAMPA WENGER MTIHANI.

Barcelona ya Spain ambao ndio mabingwa wa soka nchini humo katika kuonesha kuwa wanamhitaji kwa udi na uvumba kiungo mahiri wa timu ya Arsenal ya Uingereza Csec Fabregas, Msemaji wa klabu hiyo amefunguka na kusema kuwa wanampa Kocha wa Arsenal Mfaransa Arsene Wenger kuchagua mchezaji yeyote anaemtaka kutoka katika kikosi cha Barcelona ili amuachie Fabregas kujiunga na mabingwa hao wa Spain
                                                              Csec Fabregas
Arsene Wenger
Taarifa zimesisitiza kuwa ofa aliyopewa wWenger haihusishi wachezaji wateule wa timu hiyo ambao ni Messi, David Villa,Pique,Puyol,Xavi na kipa Valdes. Haya sasa Wakati wako Wenger kufanya maamuzi ya busara katika kuhakikisha unaiinua Arsenal ambayo kwa sasa wapenzi na mashabiki wakiwa hoi bin taaban na vipigo vya kila siku.Nimejitahidi kuwasiliana na Wenger ili nifahamu anafunguka vipi juu ya suala hili lakini simu ya ke ilikuwa busy.

No comments:

Post a Comment