Thursday, June 30, 2011

DUNIANI KUNA MAMBO.

Shabiki mwenye midadi akichezesha wachezaji.
Jamaa mmoja shabiki mkubwa wa soka alishindwa kujizuia kuhudhuria mechi ya fainali kati ya timu yake na timu pinzani, ambapo aliamua kwenda uwanjani na "controller" ili awachezeshe wachezaji anavyotaka yeye kitu ambacho ni kituko. Hali hii huwakuta mashabiki wengi hasa wale wanaojulikana kuwa na midadi,kwani shabiki mwenye midadi katika mchezo wowote ule anaweza kufanya vitu vya ajabu pale anapoenda sawa na move za mchezo sana sana mchezo wa soka, haishangazi kumuona shabiki akiyumbayumba uwanjani pale kunapokuwa na kosa kosa uwanjani na hata wakati mwingine shabiki huweza hata kupiga mashuti hewa kwa midadi ya mchezo.

No comments:

Post a Comment