Thursday, June 2, 2011

KATIKA UPANGAJI MIJI SISI TULIKUWA WAPI?

Mipango miji ni suala ambalo ni la muhimu kuliko chochote katika kuendeleza miji, kutokana na kutokuwa na umakini kwa waliotangulia na waliohusika na suala zima la usimamizi wa  upangaji miji ndio leo hii tunapata adha ya msongamano wa watu mijini iwe ni kuingia au kutoka mjini, foleni za magari tatizo hili limekuwa sugu hapa kwetu Tanzania na kutokana na jinsi ambavyo tayari mji ulivyo sidhani kama tatizo hili linaweza kutatuliwa ama kupunguzwa kwasasa na hata miaka ijayo
Ingawa tumekuwa na mapungufu katika upangaji miji tangu awali, mamlaka zinazohusika nadhani huu ulikuwa wakati wa japo kujaribu kusawazisha angalau kidogo kwa kuandaa taratibu za kutanua mji walau baadhi ya ofisi iwe ni makampuni,taasisi za serikali na zisizo za kiserikali na mashirika walau zitengewe maeneo nje ya mji ili kuondoa msongamano katikati ya jiji jambo ambalo linawapa wananchi mawazo kila inapofika asubuhi kwenda makazini na kwenye shughuli mbalimbali na pia wakati wa jioni wakiwa wanarudi.
Huwa nasikia faraja na wivu ninapoona nchi ambazo zimejipanga vyema tokea zamani ambapo hivi sasa zina mtiririko mzuri wa miji.

Pichani ni jiji la Johannesburg nchini Afrika ya kusini kama linavyoonekana katika picha hii iliyopigwa kutoka katika jengo refu kuliko yote Afrika la Carlton Tower.

Pichani ni moja ya miji ambayo ni mfano kwa jinsi ilivyopangiliwa, hili ni jiji la Barcelona nchini Uhispania.

                                       Harare,Zimbabwe.

No comments:

Post a Comment