Wednesday, June 22, 2011

UTALIPIA USD 100,000 KUNUNUA WEMBE?

USD 100,000 unaweza kuzitumia kununua vitu vingi sana na vya kifahari, unaweza nunua gari ya kifahari,boti la kifahari ama nyumba ya kisasa hivyo ni vichache tu. na kama tayari una gari yakifahari kwa mfano Audi na una boti vilevile una nyumba ya kisasa huu ni wakati wako sasa ukanunua wembe uliotengenezwa kwa madini ya sapphire, wembe unaosemekana unadumu kwa miaka 10 na makali yake yanaweza kutumika kwa miongo mingi. Sifa kubwa ya wembe huu hata kama utautumbukuza kwenye moto hauungui utabaki kama ulivyo wataalamu wanasema hata moto wa volcano hauambui kitu katika wembe huu. Kampuni iliyotengeneza wembe huu inasema ni mabadiliko kama ilivyokuwa kutoka kwenye CB Radio mpaka iPhone na sasa wembe wa kawaida mpaka kwenye hii modeli ya USD 100,000.

No comments:

Post a Comment