Tuesday, July 26, 2011

HOFFENHEIM KUIPIKU CELTIC KUMSAJILI MUSONA TOKA KAIZER CHIEFS

Timu ya Hoffeinheim ya Ujerumani ina matumaini makubwa ya kuizidi kete klabu ya Celtic ya Uskotchi katika mbio za kumuwania mshambuliaji mzimbabwe Musona mwenye umri wa miaka 21 anaekipiga Kaizer Chiefs ya kusini mwa afrika.
Musona
Katika ligi ya Afrika ya kusini iliyoisha Musona aliweka rekodi ya kufunga magoli 15 katika mechi 28 alizocheza katika ligi hiyo na kishawishi Celtic kutangaza ofa ya dau la paundi za Uingereza 2.2 milioni ili kumsajili mchezaji huyo. Lakini wajerumani wanaona Musona ndio chaguo sahihi katika kuziba pengo la Mghana Prince Tagoe waliemtoa kwa mkopo kwenda Partizan Belgrade baada ya kutofanya vizuri tangu alipojiunga na timu hiyo mwaka 2009 akiwa amefunga magoli mawili tu katika mechi 19 alizocheza katika ligi hiyo ya Ujerumani maarufu kama "Bundesliga" Ingawaje matumaini ya kumnasa Musona yanaweza kufifia kutokana na ukweli kuwa timu ya Hoffeinheim imetangaza dau dogo la paundi za Uingereza 1.3 milioni ukilinganisha na dau lililotolewa na Celtic la paundi za uingereza 2.2 milioni.

No comments:

Post a Comment