Friday, July 1, 2011

MAN CITY YAMUANDALIA NASRI PAUNDI MILIONI 20.

Samir Nasri
Bosi wa Man City Roberto Mancini anafikiria kumnyakua Samir Nasri kutoka Arsenal baada ya jitihada za kumnyakua Alexis Sanchez kukwama. Mancini anajiandaa kumpa ofa ya paundi milioni 20 na mshahara wa paundi 180,000 kwa wiki, akiwa na matumaini kuwa Nasri atashawishika na ofa hii baada ya kuachana na mpango wa kuhamia Man United.
Wenger ameshakata tamaa kumbakisha Nasri Emirates huku akiwa bado ana mkataba wa mwaka mmoja,wakati huohuo Fabrigas akihusishwa na mpango wa kwenda Barcelona.Man united bado wanamfuatilia kwa karibu Nasri huku yeye akiwa tayari ameshafanya mazungumzo na Man City.

No comments:

Post a Comment