Wednesday, July 20, 2011

NGASSA USO KWA MACHO NA MAN UNITED

Mrisho Ngassa katika moja ya mechi akiwa na timu ya Taifa

Mshambuliaji wa Azam f.c na timu ya Taifa stars Mrisho Ngassa leo anapata nafasi ya kuivaa Man United ya Uingereza ambayo ipo Marekani katika mechi za majaribio. Ngassa atakuwa na timu yake ya Seattle Sounders ya Marekani ambapo Ngassa anafanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa,kipute hicho kitapigwa katika dimba lenye nyasi bandia la Century Link. Jana Ngassa alionekana katika uwanja wa Seattle Sounders wa Starfire wakijiandaa dhidi ya mechi yao na Man United leo.
Wakati Ngassa akiivaa Man United mtanzania mwingine Nizar Khalfan akiwa na Vancouver White Caps amecheza mechi dhidi ya Man City na kupokea kipigo cha mabao 2-0.

No comments:

Post a Comment