Monday, July 11, 2011

YANGWA BINGWA KOMBE LA KAGAME

Mabingwa wa soka Tanzania Dar Young Afrikans (Yanga) wametwaa kombe la kagame baada ya kuwalaza watani wao wa jadi Simba kwa bao moja kwa uchungu katika fainali iliyopigwa katika dimba kuu la Taifa siku ya jumapili 10 julai 2011.
Katika fainali hiyo mchezo ulikuwa mzuri na wa kuviziana kwa dakika zote za mchezo,Yanga waliandika bao katika dakika ya 71 kipindi cha kwanza baada ya Kiiza kuunganisha kwa kichwa krosi iliyopigwa na Godfrey Taita lakini mshika kibendera alikataa kwa kudai kuwa mfungaji alikuwa ameotea,baada ya dakika 90 ziliongezwa dakika 30 na katika kipindi cha pili cha dakika za nyongeza alikuwa ni Rashid Gumbo aliemimina majaro safi iliyomkuta Asamoah ambaye bila ajizi alipeleka msiba Msimbazi kwa bao safi la kichwa na kumuacha golikipa Tanzania one Juma kaseja akichumpa bila mafanikio.

Asamoah muuaji katika fainali hiyo
Timu hizo zilikuwa zikikutana kwa mara ya tatu katika fainali hizo za CECAFA ambapo fainali ya kwanza ilikuwa mwaka 1975 katika uwanja wa Amani Zanzibar na yanga kuichapa Simba 2-0, zilikutana tena mwaka 1992 ambapo katika uwanja huohuo wa Amani Simba ililipa kisasi kwa kuilaza Yanga kwa penati 5-4 baada ya kutoshana nguvu 1-1 katika dakika 120, hivyo ushindi wa Yanga jana unachukuliwa kama kulipa kisasi cha miaka 20 iliyopita. Kwa ushindi huo Yanga wamelamba dola 30,000 na watani wao Simba wakiambulia dola 20,000 za ushindi wa pili.

No comments:

Post a Comment