Wednesday, August 17, 2011

ARSENAL YAANZA VYEMA LIGI MABINGWA YAISASAMBUA UDINESE


Theo Walcott

Arsenal imeweza kuizabua Udinese ya Italy kwa goli 1 kwa mtungi kwa goli maridadi la Thoe Walcott katika mechi ya kwanza ya hatua za mtoano katika ligi ya mabingwa ulaya ili kuelekea katika makundi.
Ikicheza bila nahodha wake Fabregas ambaye sasa ni mchezaji wa Barcelona ya Spain ilipata bao hilo katika dakika ya nne baada ya kazi nzuri ya Ramsey ambaye alitia majaro nzuri kabisa iliyomkuta Walcott katika nafasi nzuri ya kufunga nae bila ajizi akafanya hivyo kwa kuutia mpira kambani na kuifanya Arsenal kuwa mbele kwa bao hilo. Mchezaji wa Arsena Gibbs aliumia na nafasi yake kuchukuliwa na Djourou ambaye hata hivyo nae aliumia katika mechi hiyo.

No comments:

Post a Comment