Friday, August 19, 2011

BOB JUNIOR SIO SHOGA NI SANAA

Hivi karibuni katika vyombo vya habari vingi kumekuwa na habari ambayo imebamba vilivyo, nayo ni kumhusu mtayarishaji na msanii wa muziki wa kizazi kipya Bongo flava,huyu si mwingine ni Rais wa Masharobaro Raheem Nanji a.k.a Bob Junior, ikisemekana kwamba kukatika kwake viuno katika kazi yake ya muziki kuna uhuziano na yeye kuwa shoga, Nimeshindwa kujizuia nikiwa shabiki wake namba moja na shabiki wa sanaa ya muziki huu wa bongo flava kusikia mtu akisingiziwa vitu ambavyo havipo kwasababu ya sanaa.

Raheem Nanji a.k.a Bob Junior

Huu ni ushamba kumtafsiri mtu tofauti na vile alivyo, kukata viuno ni kazi ya sanaa kwani wacheza show za muziki huwa wanafanya nini? hata hivyo wasanii wangapi duniani wanakata viuno? mbona hata Mr Nice enzi hizo alikuwa viuno kwa kwenda mbele,je ni shoga? H Baba nae hivyohivyo,je ni shoga? Fally Ipupa nae,je ni SHOGA? Acheni kufuatilia maisha ya mtu kama mnapenda muziki pendeni muziki kama hampendi kazi zake mpotezeeni acheni kumfuatafuata katika maisha binafsi. Hata kama ni shoga yanawahusu? kuweni basi na nyinyi mashoga kama mnamuonea wivu.

Elton John na wengine maarufu ni mashoga na wapo juu ile mbaya mbona hamsemi? acheni hizo kwanza nafikiri hamjui nini maana ya sanaa au nini maana ya msanii ndio maaana mnakurupuka na kumpakazia Bob Junior. Bob Junior kama unisoma hii mzee nakushauri makamuzi ya viuno kwa kwenda mbele asiependa kazi zako na akupotezee sio lazima awe fan wako, hiyo ni sanaa na lazima msanii aheshimiwe kulingana na hisia na mawazo yake, Bob Junior be more concerned with your character than reputation, because a character is what really you are and reputation is what people think you are...wapotezeeeeeee.
Labda kwa faida ya wasiojua nini maana ya msanii au sanaa,
Kwanza Sanaa ni dhima ya upangaji wa dhana kulingana na hisia na mawazo ya msanii,
Pili Msanii sasa ndio mtu anaepanga dhana kulingana na hisia na mawazo yake.

Sasa basi Bob Junior anahaki ya kufanya kazi vile hisia na mawazo yake yanavyomtuma ili kukamilisha kazi yake ya usanii na kazi hiyo isitafsiriwe kuwa ni ushoga kwani sanaa itabaki kuwa sanaa na ushoga utabaki kuwa ushoga na ndio maana nikasema Bob Junior ameona staili ya viuno ndio inaendana na hisia zake,basi tumheshimu kama kuna mengine hayahusu katika kazi zake, au mmepandikizwa na wasanii wanaomuonea wivu kwa kazi zake naweza kuwaelewa lakini sio kiivyo.

No comments:

Post a Comment