Monday, August 22, 2011

Simba kidedea yaua 2-0,Yanga(viti maalum) yachezeshwa kwata na maafande.

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Vodacom, Yanga(viti maalum), jana walianza vibaya utetezi wao kwa kufungwa bao 1-0 na JKT Ruvu huko Morogoro Uwanja wa Jamhuri lakini Watani zao Simba walianza vyema mno huko Sheikh Amri Abeid baada ya kuichapa Timu mpya kwenye Ligi Kuu JKT Oljoro kwa bao 2-0.
Simba walifunga mabao yao yote kwenye Kipindi cha Kwanza na Straika toka Uganda Emmanuel Okwi ndie aliefunga bao la kwanza kwenye dakika ya 5 na la pili kufungwa na Kiungo kutoka Rwanda Patrick Mafisango dakika ya 15.
Mabingwa hao wa Ngao ya Jamii walichezesha Kikosi kile kle kilichotwaa Ngao ya Jamii Jumatano iliyopita walipowafunga Yanga 2-0 Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
Kwenye mechi hiyo, Mchezaji wa Simba Uhuru Selemani alirudi tena dimbani baada ya zaidi ya Mwaka mmoja kuwa nje akiuguza goti ambalo ilibidi apelekwe India kufanyiwa upasuaji.
Uhuru aliingizwa dakika ya 60 kumbadili Salum Machaku.
Huko Uwanja wa Jamhuri, Morogoro, Mabingwa Yanga walifungwa bao 1-0 na JKT Ruvu kwa bao la penati iliyopigwa na Kessy Mapande baada ya Beki wa Yanga Chacha Marwa kumfyeka Amosi Mgisa.
Kwa ujumla, Yanga walionekana goigoi katika mechi nzima.

No comments:

Post a Comment