Tuesday, September 13, 2011

AL-AHLY YATOKA SARE NA MOROCCO YAFUFUA MATUMAINI UBINGWA AFRIKA

Mabingwa mara sita wa soka barani Afrika Al Ahly ya Misri wamefufua matumaini ya kufika hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Ubingwa wa Afrika walipotoka sare ya bao 1-1 na Wydad Casablanca ya Morocco.
Wachezaji wa Al Ahly
Wachezaji wa Al Ahly

Mshambuliaji wa Misri Mohamed 'Gedo' Nagy alikuwa wa kwanza kufunga bao katika dakika ya 37 kabla ya Abderahim Benkajjane kusawazisha zikiwa zimesalia dakika mbili kabla ya mapumziko.
Nayo klabu ya Tunisia ya Esperance imeshikilia usukani  kundi B baada ya kupata ushindi mnono wa mabao 4-0 dhidi ya Mouloudia Alger ya Algeria.
Wachezaji wa Esperance ya Tunisia
Wachezaji wa Esperance ya Tunisia

Kwa matokeo hayo ni Mouloudia tu wanaoweza kufika hatua ya timu nne za mwisho za nusu fainali kutoka kundi B.
Mejdi Traore alikuwa wa kwanza kuifungia mabao Esperance katika dakika ya tisa.
Bao la pili lilipachikwa na Mkameruni Joseph Ndjeng ambaye alifanikiwa baadae kufunga mabao mengine mawili na kuhesabu mabao matatu aliyofunga peke yake.
Katika mechi za mwisho za makundi kati ya tarehe 16-18 mwezi huu wa Septemba, Ahly itakutana na Esperanace huku Wydad hawana budi kusafiri hadi Algeria kupambana na Mouloudia.
Klabu ya Enyimba ya Nigeria ilikuwa ya kwanza kufuzu hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa wa Soka barani Afrika walipoilaza Al Hilal ya Sudan mabao 2-1siku ya Ijumaa.

No comments:

Post a Comment