Thursday, October 20, 2011

WEZI WATUMIA MBINU ZA FILAMU YA BEN AFFLECK KUIBA MAMILIONI

Image icon
Sehemu ya picha katika filamu hiyo ya THE TOWN

Kuna njia nyingi za kutumia mafunzo yatokanayo na filamu sehemu mbalimbali za dunia, Mafanikio yanayovutia kutumia mbinu zake yaweza kuwa tuzo au umaarufu uliotokana na filamu hiyo, Wakati mwingine huweza kuwavutia watu kufuata yaliyomo katika filamu hizo katika kutimiza ndoto zao maishani na kwa hilo Mwandishi wa filamu ya ujangili iitwayo THE TOWN Ben Affleck anastahili kupewa heshima kutokana na filamu yake hiyo ya mwaka 2010 kushawishi makundi ya watu kutimiza ndoto zao kwa kutumia mbinu zilizotumika katika filamu hiyo kwa kufanya uhalifu na kupora mamilioni ya pesa.
T
ukio hilo limetokea huko New York nchini marekani ambapo kundi la wezi limefanikiwa kufanya uporaji wa kiasi cha dola za kimarekani 217,000 katika matukio 62, ambapo imearifiwa katika matukio hayo hawajavamia benki yeyote maeneo waliyofanya uvamizi na kupata pesa hizo ni maeneo ya biashara za kawaida na mashine za kutolea pesa"ATM".

Haya dunia ina mambo wasiwasi wangu mambo ya kuiga au kutumia mifano ya kwenye filamu isifikie kwenye zile filamu za mauaji ya kikatili kwa maana watu wote watakuwa makatili sana, nadhani kuna haja ya kuwawekea watoto wetu mipaka ya kuangalia filamu kwani ukatili,busara na huruma kwa mtoto ni muendelezo kadri anavyokua,hivyo akizoea kuangalia filamu za kikatili kuna hatari akawa mkatili kwani hisia na matendo yatakuwa yamejengeka akilini mwake.

No comments:

Post a Comment