Thursday, December 1, 2011

BARRACK OBAMA AITUMIA SALAMU ZA PONGEZI TANZANIA MIAKA 50 YA UHURU

RAIS wa Marekani, Barack Obama, ametuma salamu za pongezi na kuitakia baraka Tanzania wakati inapoadhimisha miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara.Tanzania Bara inatimiza miaka 50 ya Uhuru Ijumaa ya wiki ijayo, Desemba 9, 2011.

Rais wa Marekani Barrack Obama


Rais wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete

Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu, ilieleza kuwa Rais Obama ameihakikishia Tanzania kuwa, Marekani itaendelea kubakia rafiki na mshirika wa kuaminika katika jitihada za kuhakikisha Watanzania wanajiletea maisha bora na kwa njia za amani.

Katika salamu zake kwa Rais Kikwete, Rais huyo wa Marekani ametumia lugha ya Kiswahili kuitakia baraka Tanzania akisema “Mungu awabariki” na kufuatiwa na tafsiri ya maneno hayo kwa lugha ya Kiingereza.

Katika salamu zake, Rais Obama ameongeza kuwa umbali mkubwa wa kijiografia kati ya Tanzania, unazidi kupungua kwa sababu ya uhusiano wa karibu kati ya Wamarekani na Watanzania.

“Hali ya kuwa anuwai ya taifa lako, kama ilivyo ya kwetu, ni chimbuko na msingi wa nguvu zitakazoipitisha Tanzania katika mabadiliko mengi na changamoto nyingi zinazokabili nchi yenye demokrasia inayopanuka,” alisema Rais Obama.

No comments:

Post a Comment