Tuesday, January 24, 2012

Drogba aing'arisha Ivory Coast kombe la mataifa ya Afrika


Ivory Coast imeanza kampeni ya kunyakua Kombe la Mataifa ya Afrika kwa ushindi dhidi ya Sudan walionekana kusumbua.
Nahodha Didier Drogba alifunga bao kwa kichwa kutokana na krosi iliyochongwa na Salomon Kalou, lakini haukuwa ushindi wa kujivunia sana kwa timu inayopewa nafasi kubwa ya kunyakua kombe hilo.
Sudan itakuwa imefurahi kutokana na kandanda iliyoonesha wakati walipowasumbua Ivory Coast ambayo inajengwa na wachezaji wengi nyota wanaocheza kandanda ya kulipwa Ulaya.
Ivory Coast inamatumaini itafanya vizuri katika mchezo ujao dhidi ya Burkina Faso.
Na mshambuliaji wa Angola Manucho aliipatia ushindi Angola dhidi ya Burkina Faso katika mechi yao ya ufunguzi ya kundi B michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika.
Baada ya kosakosa za kipindi cha kwanza, Angola ilifanikiwa kupachika bao la kwanza lililofungwa na Mateus aliyetumia makosa ya walinzi wa Burkina Faso kuokoa mpira.
Alain Traore baadae akaisawazishia Burkina Faso kwa mkwaju wa free-kick umbali wa yadi 25.
Lakini mshambuliaji wa zamani wa Manchester United Manucho aliifungia bao la pili Agola baada ya kuipangua ngome ya Burkina Faso.
Bao hilo la Manucho limeifanya Angola maarufu kwa jina la Palancas Negras, kuongoza kundi B baada ya mapema Ivory Coast kupata ushindi mwembaba wa bao 1-0 dhidi ya Sudan.
Burkina Faso walitibitishwa kushiriki michuano hiyo tarehe 10 mwezi wa Januari baada ya madai ya Namibia kutupwa pale waliposema Burika faso walimchezesha mchezaji asiyestahiki katika michezo ya kufuzu.

No comments:

Post a Comment