Wednesday, February 22, 2012

NAPOLI YAINYUKA CHELSEA 3-1

Napoli imemuongezea meneja Andre Villas-Boas uchungu zaidi moyoni, baada ya kuifunga Chelsea magoli 3-1 katika mechi ya klabu bingwa ya Ulaya.
Villas-Boas
Matatizo ya meneja wa Chelsea "AVB" yanaendelea kila kukicha

Wageni Chelsea walianza kwa kufunga bao la kwanza, kupitia juhudi za Juan Mata, lakini Napoli waliweza kusawazisha.
NAPOLI 3-1 CHELSEA

Chelsea walikuwa na nafasi ya kusawazisha, lakini Lavezzi alimuadhibu David Luiz alipofanya kosa, na kuiwezesha Napoli kupata bao la tatu.
Matokeo hayo yanamaanisha “The Blues” sasa hawajapata ushindi katika mechi tano hivi karibuni, na meneja Villas-Boas yumo katika hali mbaya katika kuitetea kazi yake, huku baadhi ya wachezaji wake na mashabiki wengi wakianza kusita kumuunga mkono, na kuna wasiwasi ikiwa bado tajiri anayemiliki klabu Roman Abramovich ataendelea kuwa na subira.
Wakati huohuo, Chelsea ina matatizo zaidi, kufuatia nahodha John Terry kuumia, na huenda asicheze kwa kipindi cha wiki nane.
Terry aliumia akiwa mazoezini kujiandaa kwa mechi iliyochezwa Jumanne dhidi ya Napoli, na inaelekea huenda akapumzika hadi mwezi Aprili.
Mchezaji huyo ambaye ni stadi katika kucheza eneo la katikati ya uwanja, ataikosa pia mechi ya timu ya taifa ya England dhidi ya Uholanzi, siku ya Jumatano, wiki ijayo.
Klabu ya Chelsea imeelezea kwamba atafanyiwa upasuaji katika kipindi cha siku chache zijazo, na baada ya hapo, itafahamika vyema Terry atapata nafuu lini.
Terry, mwenye umri wa miaka 31, alikuwa pia ni nahodha wa timu ya taifa ya England, lakini mapema mwezi huu alivuliwa madaraka hayo, na tukio hilo kumfanya kocha wa timu ya taifa, Fabio Capello kuamua kujiuzulu.

No comments:

Post a Comment