Wednesday, February 15, 2012

Zambia yaingia 50 bora viwango vya FIFA, 43 Duniani ya 4 Afrika



Timu ya soka ya Zambia maarufu kama Chipolopolo wamepanda kwa nafasi 28 juu na kuingia katika 50 bora za viwango vya soka vya FIFA baada ya miaka 11 tangu ilipowahi kuwa katika 50,sasa Zambia inashika nafasi ya 4 kwa ubora wa soka barani Afrika, Zambia imepata mafanikio hayo baada ya kunyakua ubingwa wa Afrika kwa kuinyuka Ivory Coast kwa mikwaju ya penati 8 kwa 7 katika fainali kali na ya kusisimua iliyochezwa nchini Gabon katika jiji la Libraville.

Katika viwango hivyo vya soka vilivyotolewa na FIFA Ujerumani imeivuka Uholanzi na kuwa ya pili wakati huohuo Ureno(6) imepanda nafasi 1,Ivory Coast(15) imepanda nafasi 3,Mali(44) imepanda kwa nafasi 25, Ghana (23) imepanda nafasi 3 na Italy(8) imepanda nafasi 1 nazo zikipata maendeleo mazuri katika viwango vya soka Ulimwenguni.

No comments:

Post a Comment