Thursday, March 29, 2012

CCM HAINA JIPYA KATIKA MAENDELEO YA TANZANIA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Dk Jakaya Mrisho Kikwete akitafakari jambo katika moja ya mikutano ya Chama Cha Mapinduzi.

CCM Kweli ni chama kilichotuletea Uhuru na kutulea lakini sasa kimepitwa na wakati linapokuja swala la teknolojia kwani karne hii inabidi tuwe na Vitu vya karne hii.
Sasa ukiiangalia CCM ni ya zamani na sera za kizamani ndio maana Viongozi wa CCM wanashindwa kuleta mabadiliko katika nchi yetu.Kwa mtazamo wa kawaida wa umasikini uliokithiri wa watanzania,migogoro na ukosefu wa huduma bora za jamii ni dhahiri CCM imeelemewa na inaonekana kushindwa kutatua ama kuleta nafuu kwa watanzania kupitia serikali yake.

Nimesikitika sana kusikia Rais wetu Dk Kikwete akikosolewa na wataalamu wa Uchumi kutoka China na Vietnam mbele ya jamii na kadamnasi,Wakosoaji  Wameshangazwa sana na mfumuko wa bei na ubinafsishwaji wa viwanda.
Ni dhahiri kuwa ubinafsishaji wa Viwanda umetupandishia gharama za maisha kwani viwanda ndio kitu pekee kingeweza kumkomboa mkulima kwa kuongeza thamani ya mazao ya kilimo ambacho asilimia 80 ya watanzania wanakitegemea, na ajira za watanzania zingeongezeka kutokana na viwanda lakini leo hii tumebinafsisha kila kitu.

Mfano mzuri ameutoa Profesa Do DucDinh wa Taasisi ya kimataifa ya uchumi ya Vietnam kuwa Vietnam hawalimi kabisa zao la korosho lakini wana Viwanda vya kubangua korosho sasa iweje Tanzania ikose viwanda vya kubanguaimesheheni hapa nchini?
Suala la mfumuko wa bei Profesa Do Ducnh anasema mwaka jana alikuja akakuta kilo ya mchele 1,200/= leo hii kilo ya mchele 2,500/= ameshangazwa sana na mfumuko huo wa bei, Kama ugali ndio chakula kikuu halafu bei ya unga ipo juu unategemea maisha yatakuwaje? lazima yawe magumu nchi zote duniani chakula kikuu huuzwa kwa bei ya chini tofauti na vyakula vingine.

No comments:

Post a Comment