Monday, March 5, 2012

SIMBA DUME LA MBEGU OKWI,SUNZU,KASEJA WANG'AA


Felix Sunzu (kushoto) akitupia kambani goli la kwanza la Simba huku kipa na beki wa Kiyovu wakigaragara bila mafanikio

Magoli ya Mzambia Felix Sunzu katika dakika ya 19 na 32 yametosha kuifanya Simba kusonga mbele. Magoli yote yakiwa yametokana na juhudi binafsi za mshambuliaji machachari Emanuel Okwi. Kiyovu walipata goli la kufutia machozi katika dakika ya 77 kupitia kwa mshambuliaji wao Neli, Goli hilo liliwapa nguvu Kiyovu na kutaka kuongeza goli zaidi. Kama Kiyovu wangesawazisha, basi Simba wasingeweza kusonga mbele.

Mashabiki wa Simba wakishangilia bao

Simba ambayo beki yake haikuwa makini sana, ingawa waliweza kufanya maajabu kama yaliyotokea. Shukurani pia ziende kwa Kaseja ambaye kama sio jitihada zake za kuokoa michomo mikali kutoka kwa washambuliaji wa Kiyovu katika dakika za nyongeza basi tungekuwa tunaongea mengine.

Emmanuel Okwi (kulia)ambaye alikuwa mwiba mkali kwa Kiyovu katika mechi hiyo

Kwa matokeo hayo ni cheko kubwa tu kwa mashabiki na wapenzi wa Simba, huku wakimuacha mtani akiugulia baada ya kichapo cha goli moja kwa buyu kutoka kwa Zamalek huko Misri.
Mchezo uliochezwa huko Rwanda, Kigali Simba na Kiyovu zilitoshana nguvu kwa kwenda sare ya 1-1. Kwa matokeo hayo Kiyovu imetolewa kwa jumla ya magoli 3 - 2. (Simba 3-2 Kiyovu).

No comments:

Post a Comment