Wednesday, April 25, 2012

CHELSEA YATINGA FAINALI KLABU BINGWA BARANI ULAYA BAADA YA KUIADHIRI BARCELONA


Bousquets akifunga goli la kwanza la Barca

Klabu ya soka ya Chelsea ya Uingereza imefanikiwa kutinga fainali ya klabu bingwa barani Ulaya, licha ya nahodha John Terry kulimwa kadi nyekundu.

Mechi hiyo ilimalizika kwa sare ya 2-2, lakini Chelsea ikapata ushindi wa jumla ya magoli 3-2.

Andre Iniesta akitupia kambani goli la pili kwa Barca
Timu ya The Blues (Chelsea) ilionekana kuelemewa baada ya Sergio Busquets na Andres Iniesta kuiwezesha Barca kuongoza katika mchezo huo.

Lakini Ramires kwa umakridadi alifanikiwa kuichomoka ngome ya Barca na kutupia kambani bao safi la Chelsea kwa staili ya ku-chop katika mechi hiyo.



Ramires na golikipa Valdes wakishuhudia mpira uliopigwa na Ramires ukitinga wavuni

Barca walipata penalty, lakini Lionel Messi, licha ya maarifa yake na sifa nyingi katika ufundi wa penalty, lakini mkwaju huo ukagonga mwamba.


Messi akipiga penati iliyogonga mwamba

Muda wa majeruhi wa dakika tatu za nyongeza, Fernando Torres alionyesha utulivu wa hali ya juu sio tu kwa kushambulia ngome ya Barca ambayo kwa muda mrefu ilikuwa haiguswi, lakini vile vile kwa kumchenga hata kipa Valdes na kuukwamisha mpira wavuni kwa makini.

Mapema wiki hii, Torres alikuwa amenukuliwa akisema “sio siku zote timu bora hupata ushindi”, matamshi ambayo ni ndoto iliyotimia.


Torreeeeeees akimlamba chenga Valdes na kutupia kamba ya pili kwa Chelsea

Sasa vijana wa Chelsea wa Roberto di Matteo wanasubiri kufahamu kama watacheza na timu ya kocha wao wa zamani, Jose Mourinho, akiwa mkufunzi wa Real Madrid, au pengine watakutana na Bayern Munich, ambao uwanja wao ndio utakaotumiwa kuandaa fainali ya ligi ya klabu bingwa.


Nahodha John Terry akilimwa kadi nyekundu baada ya kumpiga teke Alexis Sanchez

Wachezaji wa Chelsea wakishangilia ushindi wa kutinga fainali baada ya kipyenga cha mwisho kupulizwa.

Drogba akimpoza machungu Leonel Messi

Real Madrid na Bayern zinapambana Leo, tarehe 25 Aprili 2012.

Tatizo la Chelsea ni kwamba katika fainali ya Jumamosi tarehe 19 Mei, sasa watazikosa huduma za nahodha John Terry, Ramires, Branislav Ivanovic na Raul Meireles mjini Munich, kutokana na kuadhibiwa kwa kucheza mchezo wa kuumizana katika nusu fainali.

No comments:

Post a Comment